26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

Viwanda vya Wachina Mafinga vinavyoweka rehani maisha ya wafanyakazi wao

Na Raymond Minja, Iringa

Baadhi ya wafanyakazi wa viwanda vinavyochakata mazao ya misitu wilayani Mufindi mkoani Iringa wamemuimba Rais wa Jamhuri ya mu ungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati uendeshwaji wa viwanda hivyo kwani vimekuwa vikiwe rehani maisha yao.

Moja ya kiwanda kinacholalamikiwa kuweka rehani maisha ya wafanyakazi wao ni pamoja na kiwanda cha Honghua Wood Company LTD ambacho wanasema licha ya kupewa maelekezo na viongozi wa kiserekali lakini hawajatekeleza jambo lolote.

Wametoa ombi hilo wakiamini kiongozi huyo wa juu wa nchi kwa kupitia vyombo vyake vitasaidia kuzisukuma mamlaka zinazosimia sheria za uwekezaji ili waweze kutimiza wajibu wao.

Inasemekana Februari, mwaka huu mkuu wa wilaya ya Mufindi, Saad Mtambule aliagiza kamati ya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina juu ya madai ya ukiukwaji wa haki za wafanyakazi watano wa kiwanda hicho waliopata ulemavu baada ya kujeruhuwa na mashine za kiwanda hicho wakati wakiwa kazini.

Mtambule alitoa agizo hilo mara baada ya kutembelea kiwanda hicho,kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi na menejimenti ya kiwanda na kukagua badhi ya nyaraka na kubaini mapungufu ya uendeshwaji wa kiwanda hicho.

Upungufu huo unaosemwa ni pamoja na kiwanda hicho kutokutoa mikataba kwa baadhi ya wafanyakazi,kutosajiliwa kwenye mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF).

Pamoja na agizo hilo kupewa nguvu na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Iringa, Queen Sendiga wafanyakazi hao wanalalamikia mamlaka zinazuhusika kushindwa kusimamia madai yao na kujiona yatima ndani ya nchi yao huku wawekezaji wakipewa kipaumbele.

Tarifa zinasema kati ya wafanyakazi hao yupo aliyekatika kidole,kuvunjika mguu na aliyekatwa dole gumba.

Mmoja wa wafanyakazi hao, Baraka Mlongalile alisema mguu wake mmoja ulivunjika baada ya kuangukiwa na kijiko (greda)la kuchotea mchanga.

“Ni tukio ambalo sitalisahau katika maisha yangi lilotokea September 3 Mwaka jana mkuu wa wilaya kuja kuniona na kunipa moyo,sijalipwa fidia wala haki zangu zote, ikiwemo mshahara wangu toka wakati huo alisema,” amesema Mlongalile.

Wengine wenye malalamiko yanayofanana na hayo ni Fransis Mfilinge ambaye alidai Januari, mwaka huu alikatika vidole vinne akiwa anafanya kazi kwenye kiwanda hicho.

Adani Kalenge naye alikatika vidole aliyekatika vidole vitatu naye ni moja wa wafanyakazi waliokubwa na madhila kwenye kiwanda hicho ambacho alisema mazingira wanayofanyia kazi sio rafiki kwani hakuna vifaa vya kujikingia kama kofia ngumu pamoja na gloves.

Kalenge alisema ilikuwa majira ya 8:00 machi 31, 2022 akiwa kiwandani hapo akiwa anaendelea na majukumu yake na kuvutwa na msemeno wa kukatia magogo na kukatika vidpoe vitatu.

“Tangu wakati huo mpaka sasa sijapewa fidia yoyote,na nimesimamishwa kazi na nililipwa mshahara wa mwezi wa tatu basi anasema Kalenge,” amesema Kalenge.

Pia alisema machi 31’2022 alipeleka malalamiko yake kwa mkuu wa wilaya na kuahidi kuyafanyia kazi malalamiko hayo.

Akitoa mfano, alisema kama fomu zao za madai zilipelekwa idara ya kazi Iringa mkoani Iringa (ofisi ya kazi)ili zipelekwa WCF lakini wamekuwa wakiwaambia bado hazijafika.

Wilaya ya Mufindi ni moja ya wilaya iliyobarikiwa kuwa na viwanda vingi alimaarifu (viwanda vya wachina) licha ya kutoa ajira raiya wamafinga wanaomba serekali kuingilia kati ili watu walipwe stahiki zao mana wengi wao wanaonewa ila wanaogopa kusema kwani watafukuzwa kazi na kupoteza kibarua.

Hata hivyo wanaiomba serekali kaangalia namna viwanda hivyo vinavyo nunua magogo kwani imekuwa ni staili ya kinyonyaji kwani mzigo huwa haupimwi kwa mizani bali unapimwa kwa macho kwa jina alimaarufu (Kubet).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles