32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, February 5, 2023

Contact us: [email protected]

Ofisi ya Waziri Mkuu yapokea maoni kuhusu Rasimu ya Sera ya Taifa ya Hifadhi za Jamii

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imepokea maoni kuhusu Rasimu ya Sera ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii kutoka kwa wadau wa sekta ya hifadhi ya jamii wakati wa kikao kazi kilichofanyika jengo la OSHA, leo Desemba 6, 2022, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu akitoa maelezo ya awali kwa wadau juu ya umuhimu na faida za kupitia Rasimu ya Sera ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii ya Mwaka 2022 wakati wa kikao kazi kilichofanyika jengo la OSHA, leo Desemba 6, 2022, jijini Dodoma.

Aidha, hatua ya maandalizi ya Sera hiyo mpya ni kufuatia Sera ya awali ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2003 kutofanyiwa mapitio/maboresho kwa muda mrefu, hali iliyopelekea uhitaji wa sera hiyo mpya ambayo itaendana na mabadiliko mbalimbali katika sekta ya hifadhi ya jamii.

Wadau wa Sekta hiyo wameweza kutoa maoni juu ya rasimu ya Sera ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2022 katika Kikao kazi hicho kilichoongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu.  

Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Idara ya Hifadhi ya Jamii na Idara ya Sera na Mipango zinaratibu maandalizi ya Sera ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2022.

Wadau walioshiriki kikao kazi hicho ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles