24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Bilioni 1.4 za World Vison kunufaisha maelezi ya kaya Mufindi

Na Raymond Minja, Iringa

Waziri wa mifugo na uvuvi nchini, Mashimba Ndaki, leo amezindua mradi wenye thamani ya Sh bilioni 1.4 ambazo pamoja na mambo mengine, zitatumika kununua na kuwapatia wakazi 1,200 wa Kata za Nyololo na Maduma mifugo ambayo ni ng’ombe jike 300 wenye mimba, nguruwe 600 na kuku 4,000.

Mradi huo unakusudia kukabiliana na tatizo la utapiamlo kwa Watoto pamoja na kuinua uchumi wa kaya za kata hizo chini ya ufadhili wenye tija kutoka shirika la World Vision

Akizungumza na wakazi wa kata hizo mbili, Ndaki, ametoa wito kwa wanufaika kuzingatia ufugaji bora ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji na kufuata ushauri unaotolewa na wataalamu sanjari na kuendelea kutoa ushrikiano kwa mfadhili World Vision katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi ili lengo la kuondokana na tatizo utapiamlo kwa Watoto pamoja na kuinua uchumi wa kaya

“Bajeti ijayo Serikali itawajengea majosho mawili ambapo moja litajengwa Kata ya Nyololo na lingine Kata ya Maduma pia, mwakani kweye bajeti ijayo tutajenga kituo kimoja cha kukusanya maziwa, mtaamua wenyewe kiwe hapa Nyololo au katikati ya Nyololo na Maduma, mahali ambapo wafugaji wote wataweza kufika, mtachagua wenyewe, kwa hiyo tujenge kituo ili tuweze kuwasaidia muwe wafanyabiashara wafugaji,” amesema Ndaki.

Naye Mbunge wa Jimbo la Mufindi kusini, David Kihenzile, ameliomba shirika la World Vision kupanua eneo la mradi kuzifikia Kata nyingi zaidi za ukanda wa joto na kubainisha kuwa ukanda huo wakazi wake wanachangamoto ya kiuchumi ulinganisha na ukanda wa baridi hivyo, kufikiwa na mradi huu kutachangia kuinuka kwa uchumi wa ukanda wote.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Saad Mtambule, amesema wataendelea kushirikiana na World Vision katika utekelezaji wa miradi yote wanayotekeleza katika sekta muhimu za Elimu, Afya Kilimo na Mifugo.

Awali, akisoma taarifa ya shirika, Mkurugenzi mwandamizi wa World Vision Tanzania, Dk. Paschal Mayala, ameeleza kuwa shabaha ya mradi huu ni kunufaisha watu wengi zaidi kwani kila mnufaika aliyepata ng’ombe au ngurue, kwa mujibu wa mkataba atalazimika kumgawia mtu mwingine endapo ng’ombe aliyepewa atazaa ndama Jike, lakini pia mnufaika wa nguruwe, atampatia mtu mwingine vitoto viwili vya ngurue ambavyo ni dume na Jike kwa uzao wa kwanza wa nguruwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles