22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

‘Vita ya mabao inaibeba Man United’

MANCHESTER, ENGLAND

MSHAMBULIAJI wa timu ya Manchester United, Anthony Martial, ameweka wazi kuwa, vita yao ya kupachika mabao na Marcus Rashford kutaifanya timu hiyo ifanye vizuri msimu huu.

Safu ya ushambuliaji kwa sasa itakuwa chini ya wachezaji hao wawili baada ya kuondoka kwa Romelu Lukaku aliyejiunga na kikosi cha Inter Milan wakati huu wa kiangazi.

Wachezaji hao wawili katika michezo miwili waliocheza tangu kufunguliwa kwa msimu mpya wa ligi wamefanikiwa kila mmoja kufunga mabao mawili, hivyo Martial anaamini kila mmoja kati yao wana kiu kubwa ya kufunga mabao.

Katika mchezo wao wa kwanza wa ufunguzi wa Ligi Kuu dhidi ya Chelsea, Rashford alifunga mabao mawili, huku Martial akifunga bao moja katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Chelsea, wakati huo mchezo wao wa pili dhidi ya Wolves uliomalizika kwa sare ya 1-1 Martial akifunga bao hilo.

“Kwenye mazoezi tumekuwa na ushindani mkubwa wa kufunga mabao, kila mmoja anataka kuwa kinara wa mabao, hakuna ambaye anapenda kuona mwenzake akiomuongoza kwenye kufunga bao, kuna wakati Rashford anakuwa kinara na kuna wakati ninaongoza mimi.

“Ushindani huo utakuwa vizuri tukiuendeleza kuufanya katika michezo ya ligi, hakuna ambaye atakuwa anaumia kuona mwenzake amefunga bao kwa kuwa kila mmoja ana lengo la kuisaidia timu kufanya vizuri, ninaamini kwa kufanya hivyo msimu huu tutakuwa na mabao mengi na kuisaidia timu,” alisema mchezaji huyo.

Manchester United leo watakuwa kwenye uwanja wa nyumbani na kuwakaribisha wapinzani wao Crystal Palace ambapo utakuwa ni mchezo wa tatu tangu kufunguliwa kwa msimu mpya wa ligi. Martial anaamini wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye uwanja huo wa nyumbani baada ya kutoka sare ugenini dhidi ya Wolves.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles