24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

VIRUSI VYASHAMBULIA KOMPYUTA ZA HOSPITALI

LONDON, UINGEREZA

HOSPITALI 37 za serikali nchini Uingereza zimeathirika kutokana na kushambuliwa na programu ya virusi vya kompyuta.

Shambulio hilo la tangu jana lilisababisha hospitali kadhaa za jiji la London na katika maeneo mengine kufunga mitambo yake ya kompyuta.

Madaktari wamesema licha ya kompyuta hizo kushambuliwa mtandaoni, lakini taarifa (data) za wagonjwa ziko salama.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, amesema tukio hilo ni sehemu ya shambulio kubwa lililoathiri mashirika mengine duniani kote.

Nchi karibu 100, ikiwa ni pamoja na Marekani, China, Urusi, Uhispania, Italia, Taiwan na Ujerumani zinakabiliwa na kitisho cha kushambuliwa mtandaoni.

Tukio hilo limesababisha shutuma kali kuelekezwa kwa Waziri wa Afya, Jeremy Hunt, kutokana na huduma za utabibu, ikiwamo vipimo na operesheni kusitishwa baada ya shambulizi hilo la mtandao.

Akizungumzia tukio hilo mapema jana asubuhi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Amber Rudd, alisisitiza kuwa nyaraka zote zilizohifadhi taarifa za wagonjwa zipo salama, hivyo kuwaomba watu wasiwe na wasiwasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles