29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

UGONJWA WA EBOLA WABISHA HODI DRC

KINSHASA, DRC

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, ugonjwa wa Ebola umezuka katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kwamba, hadi sasa watu watatu wamefariki dunia.

Taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) imesema kuwa, mlipuko wa ugonjwa huo umeathiri maeneo ya misitu ya Aketi, katika Mkoa wa Bas-Uele, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Shirika hilo limesema kuwa, Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Oly Kalenga, alisema kupitia barua, kulikuwa na watu tisa kutoka eneo la kiafya la Likati, Aketi waliohofiwa kuwa na Ebola.

Watano kati yao walipimwa na mmoja wao akathibitishwa kuwa na virusi hivyo. Watatu kati ya tisa hao walifariki. Waziri huyo alikuwa ameiandikia WHO barua akiomba usaidizi katika kudhibiti ugonjwa huo.

Mnamo mwaka 2014, mlipuko wa ugonjwa huo Congo DR ulidhibitiwa kwa haraka, ingawa watu 49 walifariki dunia.

Itakumbukwa kuwa, watu zaidi ya 11,000 walifariki dunia kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika eneo la Afrika Magharibi mwaka 2014 hadi 2015, hususan nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia, katika mlipuko wa Ebola uliotajwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani.

Ebola ni aina ya ugonjwa ambao mgonjwa hutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili na ambao huambukizwa mtu iwapo atagusana moja kwa moja na damu au maji maji yanayotoka mwilini mwa mgonjwa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles