25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Viongozi wa umma sasa kujaza matamko ya mali kwa mtandao

Na RAMADHAN HASSAN – DODOMA

SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma imesema kuanzia sasa viongozi wa umma watajaza fomu za matamko ya rasilimali na madeni yao kwa njia ya mtandao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu, Harold Nsekela, alisema kutokana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umm imeanza kutumia mfumo wa ujazaji wa matamko ya rasilimali na madeni kwa njia ya mtandao.

Alisema mfumo huo utawawezesha viongozi kujaza matamko yao kwa urahisi na kwa usahihi zaidi popote wanapokuwa ndani ama nje ya nchi.

“Mfumo huu utampunguzia kiongozi usumbufu wa kutumia muda mrefu kusafiri kutoka eneo lake la kazi kwenda Ofisi za Sekretarieti Makao Makuu Dodoma au Ofisi za Kanda ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za kutuma,”alisema.

Alisema wanatakiwa kutuma kupitia anuani ya barua pepe [email protected] ethicssecretariat.go.tz ili waweze kutengenezewa akaunti  za kuingilia katika mfumo huo.

Alisema taarifa zinazotakiwa ni pamoja na majina matatu ya kiongozi,( kwa kuanzia jina kwanza, kati na ukoo) namba ya simu ya mkononi, barua pepe binafsi ya kiongozi, taasisi anayofanyia kazi, cheo ama wadhifa wa kiongozi na tarehe ya uteuzi katika wadhifa ama cheo husika.

Aidha kiongozi atatakiwa kutoa taarifa ya wadhifa ama cheo alichonacho kama anakaimu ama amedhibitishwa.

Alisema viongozi wapya watatakiwa kuwasilisha taarifa zao ndani ya siku 14 baada ya kuteuliwa ama kuchaguliwa ama kupandishwa cheo.

“Viongozi watatumiwa taarifa za siri kwa njia ya ujumbe mfupi kupitia simu zao za mikononi na barua pepe  zitakazomuwezesha kuingia katika mfumo wa PDS,”alisema.

Pia aliwakumbusha viongozi wa umma kwamba kutojaza  matamko ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 15 cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma kushindwa kutoa tamko lake bila ya sababu za msingi.

“Ni imani yangu kwa kutumia mfumo huu mpya wa ujazaji wa tamko la rasilimali na madeni  kwa njia ya mtandao na zoezi hilo litafanyika kwa wakati,”alisema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,540FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles