23 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Shein aongoza kumbukumbu ya Karume, corona ikitawala

Na Mwandishi wetu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, amejumuika na viongozi  wa Serikali na wa madhehebu ya dini katika dua ya kumbukumbu ya muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Mzee Abeid Amani Karume.

Hafla hiyo ilifanyika kwenye Kaburi la kiongozi huyo liliopo Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui, ambapo viongozi wa madhehebu ya dini walipata fursa ya kumuombea dua marehemu.

Akifungua dua ya kiislamu, Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi, alimtakia malazi mema kiongozi huyo na kusema wakati wa uhai akiwa Rais wa Zanzibar, Marehemu alizingatia umuhimu wa kuweka hali sawa za wananchi wake na kuhakikisha wanaishi katika makaazi bora.

Alimuomba Mungu kuinusuru Zanzibar na dunia kwa ujumla ili kuondokana na maradhi ya corona yaliosambaa Ulimwenguni.

Naye, kiongozi wa Kanisa la Anglicana Zanzibar, Askofu Michael Henry Hafidh, alimtakia msamaha, rehema na amani kiongozi huyo katika malazi yake, sambamba na kumuomba Mungu kubainisha njia ya kuondokana na ugonjwa wa corona dunia.

Aidha, kiongozi wa jamii ya Kihindu Yoges Pirocit alitumia fursa hiyo kumuombea dua na kumtakia rehma kiongozi huyo.

Dua ya kumbukumbu ya Abeid Karume, ambayo kwa hufanyika kila April 7, ilihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa, viongozi wakuu wa kitaifa wastaafu akiwemo Dk. Amani Abeid Karume na baadhi ya mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Wengine waliohudhuria dua hiyo ni kiongozi wa Mabalozi wadogo waliopo Zanzibar George Augostino, mwakilishi wa familia ya marehemu, Balozi Ali Karume, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Abdalla Juma Sadalla ‘Mabodi’.

Dua ya kumbukumbu ya marehemu Mzee Karume mwaka huu imehusisha washiriki wachache, ikiwa tofauti na ilivyozoeleka  ambapo wananchi na waumini walipata fursa ya kushiriki na kusoma khitma, hatua hii ikiwa ni juhudi za kukabiliana na maambukizo ya virusi ya corona vinavyoendelea kusambaa duniani kote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles