30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wa Dini hamasisheni matumizi ya nishati safi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

VIONGOZI wa dini nchini wameombwa kushiriki kikamilifu katika kuihamasisha jamii kutumia nishati safi ya kupikia ili kuondokana na uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi ya kuni na mkaa katika kuandaa chakula.

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Oryx Gas Shaban Fundi akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Benoit Araman wakati wa hafla ya kukawa mitungi ya Oryx 1,000 kwa viongozi wa dini na wajasiriamali wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Wito huo umetolewa leo Februari 27, 2024 na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi ya Oryx 1,000 pamoja na majiko yake kwa viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali mkoani Kilimanjaro yaliyokwenda sambamba na utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya matumizi ya nishati safi ili kuepuka madhara kwa jamii.

Kapinga ametoa wito huo wakati wa kukabidhi mitungi hiyo kwa viongozi wa dini na wajasiriamali ambapo amesema viongozi wa dini wanamchango mkubwa katika kusaidia jamii kutambua umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuachana kutumia kuni na mkaa.Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania, Shaban Fundi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Benoite Araman ametumia nafasi hiyo kueleza kwa muda mrefu sasa wamekuwa wanajivunia kuwezesha makundi mbalimbali yakiwemo wanawake, watoto na wajasiriamali kupata nishati safi ya kupikia.

Amesema kwa kufanya hivyo wanaamini wanaikomboa jamii na Taifa kwa ujumla wake kwani kupika kwa gesi ya Oryx kuna maanisha kuboresha afya za kinamama kwa kuepuka kuvuta moshi mbaya wa kuni na mkaa. Pia tunaweza watoto kupata muda wa kwenda shule badala ya kutumwa kutafuta kuni,” amesema Fundi.

Aidha, amekumbusha kuwa mwaka 2021 Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alianzisha kampeni ya nishati safi ya kupikia na alitoa maono yake ya kwamba ifikapo mwaka 2032 asilimia 80 ya wananchi itumie nishati safi, hivyo kuanzia hapo Oryx iliongeza nguvu na hadi sasa zaidi ya mitungi 19,000 bure yenye thamani isiyopungua Sh bilioni 1.5.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa dini ambao wamepatiwa mitungi ya gesi sambamba na kupatiwa mafunzo ya matumizi salama ya nishati hiyo, wamemshukuru mbunge Shally pamoja na Oryx kwa kutambua kundi hilo na nafasi yake katika kuhamasisha jamii kutunza mazingira kwa kutumia nishati safi ya kupikia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles