29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Shule za Wasichana ziwe mkombozi kwa watoto wa kike nchini

Na Mwandishi Wetu, Korogwe

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa Rehema Sombi amewataka wanafunzi wa kike kutumia fursa ya shule za wasichana za mikoa kuinua kiwango cha elimu sambamba na ufaulu.

Sombi ametoa wito huo leo Februari 27, 2024 wakati wa ziara ya wajumbe wa kamati ya utekelezaji Taifa walipotembelea shule ya sekondari ya Swisho wa shamba wilayani Korogwe.

Amesema maono ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kujenga shule za wasichana nchi nzima ni kutoa fursa kwa wasichana wengi kupata elimu na hivyo kuweza kuja kulitumikia Taifa hapo baadae.

“Taifa linawategemea, hivyo niwaombe itumieni fursa ya shule hizo kupata elimu na hivyo kuweza kulisaidia kupata wataalamu wengi zaidi lakini kuongeza kiwango cha wahitimu wakike,” amesema Sombi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles