25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wa Democrat, Republican walumbana kesi ya Trump

WASHINGTON, MAREKANI

VIONGOZI wa Republican na Democrats katika Bunge la Seneti nchini Marekani wamelumbana kuhusiana na kanuni zitakazofuatwa katika kesi inayomkabili Rais Donald Trump inayotakiwa kuwasilsihwa kwenye Bunge le Seneti.

Democrats wanataka hakikisho kwamba mashahidi na baadhi ya stakabadhi muhimu zitaruhusiwa ili kuruhusu kile ambacho wanakitaja kuwa kesi ya haki.

Kiongozi wa Democrats Chuck Schumer alisema kwamba ufichuzi wa barua pepe kuhusu msaada wa Ukraine ni kumbusho kuhusu kwa nini uwazi unahitajika, lakini hakukubaliana kuhusu iwapo mashahidi wataruhusiwa kutoa ushahidi wao wakati wa kesi hiyo.

Rais Trump alipigiwa kura ya kutokuwa na imani naye katika Bunge la Uwakilishi (Congress) wiki iliopita kwa matumizi mabaya ya mamlaka na kulizuia bunge la uwakilishi, hivyo kuwa Rais wa tatu katika historia ya Marekani kushtakiwa.

Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa kwamba hataondolewa ofisini kwa kuwa chama chake cha Republican kina maseneta wengi katika bunge hilo ambapo kesi hiyo itafanywa kama ilivyo kulingana na Katiba.

Kesi hiyo inatarajiwa kuanza mwezi ujao baada ya likizo kukamilika. Lakini wana Democrats kufikia sasa wamekataa kutoa stakhabadi za kesi hiyo iliyopigiwa kura na Bunge la Uwakilishi na sasa itarajiwa kuwasilishwa katika Bunge la Seneti.

Wanataka hakikisho kutoka kwa McConnell kwamba mashahidi wao waliowachagua,  karibia wanne wakiwa wafanyakazi wa sasa na wa zamani wa Ikulu wakiwa na ufahamu kuhusu kilichotokea Ukraine, wataruhusiwa kutoa ushahidi.

Trump anatuhumiwa kwa kumshinikiza Rais wa Ukraine kuanza uchunguzi dhidi ya mpinzani wake wa kisiasa, mgombea wa Chama cha Democrat, Joe Biden.

Juzi Jumatatu, McConnell aliambia kitengo cha habari cha Fox News siku ya Jumtatu kuwa hawajakataa mashahidi lakini atasimamia kesi kama ile iliyomkumba aliyekuwa Rais wa Marekani, Bill Clinton mwaka 1999, ambapo maseneta waliamua ni mashahidi gani watakaoitwa baada ya kufungua mjadala na maswali.

McConell alimshutumu Spika wa Bunge la Uwakilishi, Nancy Pelosi kwa kushikilia nafasi na kusema kwamba anajaribu kuwaeleza jinsi ya kuendesha kesi hiyo katika Bunge la Seneti.

Chuck Schumer alisema kwamba yeye na mwenzake wa Republican wapo katika mkwamo baada ya kufanya mkutano muhimu siku ya Alhamisi ili kuzungumzia sheria za kesi hiyo.

Wakati wa mkutano na wanahabari nyumbani kwake huko New York siku ya Jumapili, Schumer alisema kwamba Republicans hawajatoa sababu muhimu kwa nini hakupaswi kuwepo kwa mashahidi na kwa nini stakhabadhi hazifai kutolewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles