25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Mpelelezi wa UN akosoa uamuzi wa kesi ya Khashoggi

NEW YORK, MAREKANI

MPELELEZI wa Umoja wa Mataifa (UN), Agnes Callamard, alisema hukumu ya kifo kwa watu watano nchini Saudi Arabia kutokana na mauaji ya mwandishi wa habari wa Kisaudia, Jamal Khashoggi, imesababisha hasira ulimwenguni kwa sababu wahusika halisi wa tukio hilo bado wapo huru.

Callamard, mchunguzi maalumu wa UN aliyechunguza kifo cha Khashoggi, alisema atahakikisha kuwa hakuna mtu, bila kujali wadhifa au nguvu alizonazo, atakayeepuka kuwajibishwa iwapo alihusika na mauaji hayo.

Khashoggi, mwandishi wa habari aliyekuwa wakati mmoja karibu na familia ya kifalme ya Saudia, aliuawa na viungo vyake kukatwakatwa ndani ya ubalozi wa nchi yake mjini Istanbul, Uturuki, mwaka jana.

Siku ya Jumatatu, mahakama mjini Riyadh iliwahukumu watu watano kwa mauaji ya mwandishi huyo wa habari.

Mpelelezi wa Umoja wa Mataifa, Agnes Callamard alipozungumza na Shirika la Habari la Ujerumani (DPA) aliyataja maamuzi katika kesi hiyo kuwa ni kejeli na kwamba anataka haki itendeke.

Callamard ametaka Saudi Arabia isipewe nafasi ya kuandaa mkutano wa kilele wa G 20 mwaka ujao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,430FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles