24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Vikwazo vya Marekani dhidi ya makampuni ya China

WASHINGTON, MAREKANI

WAZIRI wa Ulinzi wa Marekani, Mark Esper anapanga kufanya ziara nchini China kwa mazungumzo juu ya vipi nchi hizo mbili zinaweza kuweka sawa mawasiliano yao katika mzozo wakati hali ya wasi wasi kimkoa kati ya mataifa hayo yenye nguvu duniani ikiongezeka na wasi wasi ukizidi kuhusiana na eneo linaloweza kuleta mzozo wa bahari ya kusini mwa China.

Esper alisema jana kuwa anamatumaini kufanya ziara hiyo kabla ya mwaka kumalizika kuweka mfumo ambao utakuwa muhimu kwa ajili ya mawasiliano wakati wa mzozo na kuimarisha nia zao za kukamilisha kwa uwazi mfumo wa kimataifa ambao nchi hizo zote zimo. 

Wakati huo huo China imesema jana kuwa itachukua hatua muhimu ambazo hazikutajwa, baada ya serikali ya Marekani kuweka vikwazo dhidi ya makampuni 11 inayosema zinahusika katika ukiukaji wa haki za binadamu katika jimbo la magharibi mwa China lenye Waislamu la Xinjiang. 

Hata hivyo Marekani iLIiamuru leo China kufunga ubalozi wake mdogo mjini Houston, China imesema leo, katika kile ilichosema ni uchokozi wa kisiasa, ambao utaathiri zaidi mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizo.

AP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles