24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Vijana watakiwa kugombea nafasi za uongozi

Amina Omari-Muheza

VIJANA wametakiwa kuchangamkia fursa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi vyama vya siasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, pamoja na Uchaguzi Mkuu mwakani.

Hayo yalisemwa jana na Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Muheza, Salome Zuakuu wakati akizungumzia maandalizi ya sherehe ya uzinduzi ya Muheza ya Kijani ambayo itafanyika mwishoni mwa wiki.

Aliwataka vijana wenye sifa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi huo ili kuweza kuonyesha uwezo wao wa kuongoza.

“Kwa kasi ya Serikali ya sasa, inahitaji nguvu kazi ya vijana hivyo niwaombe vijana wajitokeze katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuweza kupata fursa ya kutumikia wananchi kwa kasi zaidi,” alisema Zuakuu.

Alisema Muheza ya Kijani ina lengo la kuhakikisha wanajipanga kuhamasisha vijana kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chama.

Katibu wa CCM Wilaya ya Muheza, Mohamed Moyo, alisema kuwa maandalizi ya uzinduzi wa Muheza ya Kijani yanakwenda vizuri

Alisema kuwa mpango huo wa uzinduzi unakwenda kuondoa dhana ya kwamba nafasi za uongozi ni za kada fulani ya watu kumbe ni dhana ambayo imepitwa na wakati kwa sasa.

“Kuna dhana imejengeka kwa wananchi kwamba nafasi za uongozi ni watu fulani lakini kwa awamu ya hii tunakwenda kuvunja hiyo dhana  na tunataka viongozi ambao wataweza kuwajibika kwa wananchi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles