27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli awatumbua DC, Mkurugenzi Malinyi

Mwandishi Wetu

Rais Dk. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro, Majura Kasika na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mussa Mnyeti.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, imesema Uteuzi wa viongozi hao umetenguliwa kuanzia leo Jumanne Septemba 17 na uteuzi wa viongozi watakaojaza nafasi hizo utafanyika baadaye.

Jana Septemba 16, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimuelekeza Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, kwenda kuchunguza weledi wa utendaji kazi wao baada ya kuchukizwa na mgongano uliopo baina ya viongozi hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles