23.8 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Vijana Kilombero wahimizwa kujikwamua kiuchumi

Na Mohammed Ulongo, Mtanzania Digital

Wakazi wa Kidatu Wilaya ya Kilombero mkoani Mororgoro wameshiriki katika uzinduzi wa Ofisi ya kikundi cha Mazingira ni Uhai itakayohudumia kata sita za wilaya hiyo huku wakiaswa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la Sensa Agosti 23, mwaka huu.

Mdau wa Mazingira, Abdon Mapunda(katikati) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo.

Wito huo umetolewa Juzi na Mdau wa Mazingira, Abdon Mapunda wakati wa hafla ya uzinduzi huo ambapo pia amewasihi vijana kutumia kikundi cha Mazingira ni Uhai kujiwezesha kiuchumi ikiwamo kupeana mikopo.

“Tumezindua ofisi hii ambayo tunaamini kwamba itakuwa msaada kwa kata zote sita wilaya ya Kilombero, hivyo pamoja na mambo mengine niwahisi vijana kutumia kikundi chenu hiki cha Mazingira ni Uhai kwa ajili ya kujiwezesha kiuchumi kwa kupeana mikopo itakayowainua.

“Pamoja na hilo, niwasihi tumuunge mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujitokeza kuhesabiwa katika Sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 23, 2022 nchi nzima, kwani kufanya hivyo kutairahisishia Serikali kuwa na takwimu sahihi zitakazosaidia kupanga mipango ya maendeleo,” amesema Mapunda.

Mwenyekiti wa kikundi hicho cha Mazingira ni Uhai, Issa Mahuhu amewataka wana-Kilombero kuchangamkia fursa hiyo kwa kujiunga na kikundi hicho ili kuweza kushiriki katika harakati za utunzaji wa mazingira pamoja fursa zilizopo.

Upande wake Diwani wa kata ya Kidatu, Hilda Maimbali amesema amefurahishwa na uzinduzi huo huku akisisitiza kuwa zoezi hilo ni la kwanza katika wilaya ya Kilombero lenye kata 19 huku akiwasisitiza wananchi kushirikiana katika kutunza mazingira.

Naye Afisa Maendeleo wa kata ya Kidatu, Pili Ramadhani amepongeza mpoango huo na kwamba utakuwa na tija kubwa ndani ya kata hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles