27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali, FAO waja na mkakati wa kudhibiti udumavu nchini

*Watoto wa kike kujengewa uwezo tangu wakiwa elimu ya msingi

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) kupitia mradi wa Agri-Connect imeandaa mkakati wa kukabili udumavu nchini kwa kuwajengea uwezo watoto wa kike 17, 000 wa shule ya msingi nchi nzima namna ya kuandaa mlo kamili tangu wakiwa shule.

Mpango huo ambao unatarajiwa kudumu hadi mwaka 2023 pamoja na faida nyingine unalenga kupunguza kiwango cha udumavu hapa nchini kutoka asilimia 32 ya sasa.

Akizungumza Dar es Salaam Julai 30, 2022 kwenye semina maalumu iliyolenga kuwapa elimu watoto wa kike kwenye shule tano ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam kupitia Taasisi ya Girl Guide Association, Mwakilishi Msaidizi wa FAO, Charles Tulai almefafanua kuwa mradi huo umewalenga watoto wakike kwani wanapofikia umri wa kujifungua hukumbwa na changamoto nyingi za uzazi.

“Mradi huu umewapa kipaumbele watoto wa kike kwani wakipewa elimu ya lishe ndio mzizi wa kukata udumavu kwenye familia. Tumeamua kutekeleza mradi huu kwenye kundi hili tangu wakiwa wadogo kwasababu wakati wa kujifungua wanakumbwa na matatizo ya upungufu wa damu, kupoteza maisha na mtoto kuzaliwa na uzito mdogo.

“Hivyo kumuandaa mtoto wa kike tuna uhakika atatunza familia yake na akizaa atakuwa na mtoto mwenye afya nzuri na hata shuleni mtoto huyu atakuwa na akili na atafanya vizuri kwenye masomo yake,” amesema Tulai.

Upande wa Serikali kupitia kwa Afisa Kilimo Mkuu na Mratibu wa Lishe Wizara ya Kilimo, Margaret Natai mesema kupitia mradi huo wamelenga kuhamasisha watoto wa kike kuzalisha mazao yanayofaa kwa ajili ya lishe na namna ya kuandaa chakula.

“Kwa hapa Dar es Salaam tumeanza na wasichana 200 lakini mradi huu utawafikia wasichana 17,000 katika kanda mbalimbali ikiwamo Nyanda za Juu Kusini ukilenga kwenye uanzishwaji wa bustani shuleni, kutuoa ujumbe kwenye vyombo vya habari, kuanzisha majiko kuelimisha kina mama ngazi ya vijiji namna ya kuandaa vyakula, kwani changamoto iliyo nchini nchini siyo chakula bali namna ya kuandaa,” amesema Natai.

Ameongeza kuwa mradi huo wenye kaulimbiu ya Lishe bora ni mtaji utawajenga watoto wakike tangu wakiwa wadogo lengo likiwa ni kuwapa uelewa wa namna bora ya kula ili watakapojifungua wawe na watoto wenye afya nzuri.

“Asilimia 32 ya watoto wanaudumavu nchini, Wizara ya Kilimo lazima tushushe kiwango hiki tumekuja na mbinu ya namna ya kushusha kiwango hicho cha udumavu, tunataka kuunganisha kilimo na lishe,” amesema na kuongeza kuwa mradi huo unaingizwa kwenye mikakati na sera za wizara hiyo.

Grama ya mradi huo kwa upande wa lishe itagharimu Euro 2,150,000 ambapo kati ya hizo zipo zinazotolewa na Umoja wa Ulaya(EU).

Upande wake Kinara wa Lishe Bora ni Mtaji Bara na Visiwani kutoka kampuni ya Open Kitchen, Upendo Mwarongo amesema kampeni hiyo inalenga kuwafundisha na kuwahamasisha kuwa bustani siyo lazima mtu awe na shamba kubwa kwani anaweza kufanya hivyo kwa kutumia makopo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles