27.4 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Chongolo awataka Wananchi kutunza chakula

Na Safina Sarwatt, Siha

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Daniel Chongolo amewataka wananchi kutunza chakula kilichopo kwani maeneo mengi yameshindwa kuzalisha kutokana na mabadiliko ya tabianchi na ukame.

Chongolo ameyasema hayo Agosti 2, 2022 katika ziara ya kikazi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro na kuongeza kuwa maeneo mengi mwaka huu yameshindwa kuzalisha chakula kutokana na ukosefu wa mvua.

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo(Kulia) akizungumza mapema Agosti 2, 2022 mkoani Kilimanjaro.

Amesema ni vyema wananchi wakatunza chakula kilichopo kwa ajili ya familia zao na kwamba huko mbele chakula kitapanda bei maradufu.

“Kila mmoja aweke akiba ya chakula alicho nacho, atumie vizuri kwa ajili ya familia yake kwani huko mbele tuendako kutakuwa na upugufu wa chakula, kitauzwa kwa bei kubwa ambapo itakuwa ni changamoto kwa kila mmoja kumudu,” amesema Chongolo.

Aidha, Chongolo amezitaka Halmashauri zote nchini kuweka utaratibu wa kuhamasisha wananchi mpango wa upandaji miti ili kuboresha mazingira.

Akizungumzia suala ya barabara ya Bomang’ombe -TPC ameahidi itajengwa kwa kiwango cha lami na kufunguliwa kwake kutafungua fursa za kiuchumi na kupunguza msongamano wa magari katika barabara kuu ya Moshi-Arusha.

Wakati huo huo Chongolo amewataka wananchi kutumia fursa za utalii kwa kuanzisha vikundi vya utamadumi wa asili.

Upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Uviko-19 pamoja na kupata chanjo kwa wale ambao hawajachanja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles