23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

VIJANA IKUNGI WAOMBA MIZINGA YA NYUKI

Na NATHANIEL LIMU-IKUNGI


SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, imeombwa kuangalia uwezekano wa kuwakopesha vijana mizinga ya nyuki ya kisasa ili waweze kujiajiri kwenye ufugaji nyuki kibiashara.

Ombi hilo limetolewa juzi na vijana 30 wenye umri chini ya miaka 30 na wakazi wa Wilaya ya Ikungi ambao wanahudhuria mafunzo ya ufugaji nyuki kibiashara kwa nadharia na vitendo.

Mafunzo hayo yalifadhiliwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la SEMA, yanayoendelea kwenye shamba la nyumba ya nyuki lililopo katika Kijiji cha Nkuninkana Kata ya Puma.

Vijana hao walisema Serikali imefanya vizuri kumtambua mdudu nyuki kwa kuanzisha na kutunga sera, sheria na  vyuo mbalimbali vinavyotoa elimu kwa undani juu ya ufugaji wa nyuki.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Godfrey Peter, alisema umefika wakati sasa Serikali ianzishe kitengo maalumu cha kukopesha mizinga ya kisasa kwa wahitimu mbalimbali wa mafunzo ya ufugaji nyuki.

“Serikali ya Dk. John Magufuli imefanya mambo mengi mazuri ikiwamo vijana wengi kujitambua na kuanza kujituma kwa bidii. Tunaomba kupitia mafunzo haya tunayopewa na shirika la SEMA, tukopeshwe mizinga mitano ya kisasa, kuanzia hapo kila mmoja na familia zetu vipato vitaongezeka,” alisema Peter.

Alisema SEMA wamewafundisha juu ya hasara ya kufuga nyuki kizamani na faida za kufunga nyuki kibiashara na juu ya mazao saba ya nyuki ambayo mengi walikuwa hawayafahamu.

Ofisa  nyuki wa Halmashauri ya Ikungi, Filbert Benedict, ameipongeza SEMA kwa uamuzi wake wa kusaidia vijana kujiajiri kwenye ufugaji nyuki kibiashara ili waweze  kujikomboa kiuchumi na kuongeza kuwa asilimia 70 ya ardhi yake inafaa kwa ufugaji nyuki.

Awali Ofisa Mradi wa fursa za ajira kwa vijana (OYE), Salumu Hassani, alisema vijana waliopata mafunzo hayo wanatarajiwa kuanzisha vikundi na taasisi za biashara ili kupata mitaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles