24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Vigogo wapishana urejeshaji fomu za maadili

Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

WAKATI leo ikiwa mwisho wa uwasilishaji fomu za tamko la mali na madeni viongozi mbalimbali wamepishana kuwasilisha taarifa zao katika ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika mikoa mbalimbali nchini.

Katika ofisi za Kanda ya Dar es Salaam Mtanzania iliwashuhudia viongozi kadhaa wakipishana wakiwamo makatibu wakuu, wakurugenzi na madiwani ambao kila mmoja alikuwa akipota kuwasilisha fomu ikiwa ni utekelezaji wa agizo hilo kwa mujibu wa sheria za nchi, ambapo wanatakiwa kufanya hivyo hadi kufikia leo 31, 2019.

Ikiwa watabainika ambao watashindwa kufanya hivyo ni watakuwa wakikabiliana na makosa ya kimaadili.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekele, alisema kuwa licha ya kutokuwa na takwimu rasmi lakini mwitikio umekuwa mzuri katika ofisi zote za kanda na kwamba leo unatarajiwa kuwa mzuri zaidi.

“Kutowasilisha tamko ni kosa la kimaadili na sheria iko wazi kuwa kama mtu asipowasilisha kwa sababu zisizo za msingi, utaona kumbe sheria imeweka sababu za msingi ambazo mtu anaweza asiwasilishe tamko kwa wakati,” alisema Jaji Nsekela.

Alipoulizwa kuwa sheria imeelekeza lini kiongozi wa umma anapaswa kuwasilisha tamko hilo, Jaji Ndekela alisema kuwa kwa bahati mbaya sheria haijaweka wazi suala hilo na kwamba wao wanaona kuanzia Oktoba ni muda mzuri wa kufanya hivyo.

“Ujazaji wa tamko hili uko mara tatu, ukipewa wadhifa unajaza, unapostaafu unajaza kwaheri lakini kama hapo katikati, hujapewa wadhifa na hustaafu unatakiwa ujaze.

“Ukiniuliza kwanini hawajazi mapema sina jibu huenda ni hulka zetu kwa sababu wajibu wetu tunaujua kwa sababu tunapopewa wadhifa tunajaza tamko,” alisema Jaji Nsekela.

Akitoa wito kwa viongozi kuelekea mwakani ambapo kutakuwa na Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani alisema kuwa licha ya kwamba bado ni mapema na kuna mamlaka zinazopaswa kulizungumzia hilo ikiwamo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) lakini ni vema viongozi wakawa watu wenye maadili kwa sababu ndilo msingi wa kila kitu.

“Viongozi tusiwe na madoa madoa tuwe na maadili katika jamii,” alisema Jaji Nsekela.

JPM AREJESHA

Desemba 29, mwaka huu Rais Dk. John Magufuli aliwasilisha tamko linalohusu mapato, rasilimali na madeni ya viongozi katika Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa umma ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kisheria na kikatiba.

Tamko hilo liliwasilishwa na Katibu wa Rais, Ngusa Samike ambaye alitumwa na Rais Magufuli ambaye yupo mapumzikoni wilayani Chato na limepokelewa na Kamishna wa Sektretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kupokea tamko hilo Jaji Nsekela, alisema kitendo alichokifanya Rais Magufuli,  kimetekeleza takwa la kikatiba Ibara ya 132 (5) (D) linalowataka viongozi kuwasilisha taarifa za tamko la mapato, Rasilimali na madeni mara kwa mara lakini pia ametekeleza sheria no 13 ya mwaka 1995 kingu cha 9.

Kutokana na hali hiyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wengine kutumia siku 2 zilizobaki kufanya hivyo kabla ya leo Desemba 31, mwaka huu katika kutekeleza takwa hilo la kisheria na kikatiba.

WAJIBU WA SEKRETERIETI YA MAADILI

Sekretarieti  ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilianzishwa  kwa mujibu wa  ibara  ya  132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na ni  Idara  ya  Serikali  inayojitegemea  chini ya Ofisi  ya  Rais ambapo ilianza  kazi  zake  rasmi   Julai   mwaka   1996.

Sekretarieti   ya  Maadili  ilianzishwa  ili  kutekeleza  Sheria  ya  Maadili ya Viongozi wa Umma, Na. 13 ya mwaka 1995  kama  ilivyo  rekebishwa  na  Sheria  Na.  5  ya  mwaka 2001.

 Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilitungwa na  Bunge ili kutekeleza matakwa ya Katiba ya Jamhuri  ya  Muungano wa Tanzania ya 1977,  ibara  ya 132 (4) ambayo  inasema  kuwa  Bunge  litatunga Sheria itakayoainisha  misingi  ya  Maadili  ya  Viongozi  wa  Umma  itakayozingatiwa  na  watu  wote  wanaoshika  nafasi  za  madaraka  zitakazotajwa na Bunge.

Pia, katika Ibara 132 (5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ililipa Bunge mamlaka ya kuweka misingi ya Maadili ambayo:(a)   Itafafanua   nafasi   za   madaraka   ambazo  watu  wenye kushika  nafasi  hizo  watahusika nayo;(b) Itawataka watu wanaoshika  nafasi  fulani  za  madaraka  kutoa  mara kwa mara maelezo rasmi kuhusu      mapato, rasilimali na madeni  yao;(c)  Itapiga marufuku mienendo na tabia inay opelekea kiongozi kuonekana hana uaminifu, anapendelea au si muadilifu au  inaelekea kukuza au kuchochea rushwa katika shughuli za umma au inahatarisha  maslahi au ustawi wa jamii.

Na kifungu (d)  Itafafanua adhabu zinazoweza kutolewa  kwa  kuvunja misingi ya maadili;(e)  Itaelekeza taratibu, madaraka na desturi  zitakazofuatwa ili kuhakikisha utekelezaji  wa maadili;(f ) Itaweka masharti mengine yoyote yanayofaa au ambayo ni muhimu kwa madhumuni ya kukuza na kudumisha ua minifu, uwazi, kutopendelea na uadilifu katika  shughuli  za  umma  na  kwa  ajili  ya  kulinda  fedha  na  mali  nyingi

Hata hivyo kayika kuleta ufanisi katiika kukuza uchumi wan chi inaelezwa ni muhimu kwa  viongozi waliopewa jukumu la  kuongoza  umma,  kuwa  na  maadili  katika   utendaji   wao  wa  kazi za kila siku wanazozifanya kwa manufaa ya   wananchi, lengo kuu ni  kuwaongoza wananchi katika misingi ya haki na  usawa katika kuwaletea maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles