Utalii wa ndani wapigiwa chapuo

0
535

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

SEKTA ya utalii ni muhimu kwa uchumi wa nchi, ambapo kutokana na hali hiyo Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), imesema itaendelea kusapoti sekta ya utalii nchini kutoka na mchango wake katika kuinua pato la taifa, imeelezwa jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana, Meneja Chapa na Mawasiliano wa benki hiyo, David Raymond alisema imekuwa kwa kipindi kirefu ikiweka juhudi mbalimbali ili kuhakikisha sekta ya utalii pamoja na mnyororo wake wa thamani ukifanikiwa.

“Mfano ni kupitia kampeni yetu ya Ibuka Kidedea, na zawadi mbalimbali, tunapeleka washindi wetu wane Hifadhi ya Taifa Serengeti ili kuona vivutio vya kipekee ambavyo si rahisi kuviona mahali pengine.

“Hii ni moja ya juhudi za benki kusapoti utalii wa ndani, tunajua ni nafasi nzuri kwa wateja wetu na wenza wao kupata nafasi hii ya mapumziko katika mwisho wa mwaka,pia kwa tukio hili kwa namna nyngine tutakuwa tukisaidia juhudi za serikali yetu katika kutangaza utalii wa ndani na vivutio vya mbuga zetu za wanyama”, aliongeza Bwana Raymond.

Naye Meneja wa Bidhaa za Uwekezaji wa benki hiyo, Dorothea Mabonye alisema imewekea kwa kiasi kikubwa katika bidhaa za kidigitali katika kuhakikisha wateja na wasio wateja wanafikiwa na huduma za benki hiyo mahali walipo.

“Ni matumaini yetu washindi wa ibuka kidedea watafurahia safari hizi za kitalii na pia wataweza kufurahia huduma zetu kwa njia za kidigitali popote watakapokuwa,” alisema.

Mmoja wa washindi wa Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Esther Ndunguru anayekwenda kufaya utalii wa ndani Hifadhi ya Serengeti na mwenza wake, alisema amefurahishwana safari hiyo na kuwataka Watanzania na wateja kujiunga na akaunti ya Malengo ya benki hiyo ili nao waweze kupata bahati kama yakwake.

Washindi walioshinda safari ya Serengeti ni,  Christopher Mgote kutoka Nzega,  Makongoro Makongoro kutoka Arusha, Jocelyine Rwechengura na Esther Ndunguru wote kutoka Dar es Salaam.

Washindi walioshinda safari ya Sychelles ni, Wambura Wambura kutoka Tarime mkoani Mara, Ramadhan Saidi, Lettice Ruta

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here