Vifuaviwili aiomba serikali iongeze nguvu

0
742

Glory Mlay -Dar es salaam

BONDIA wa kulipwa nchini, Bruno Tarimo ‘Vifuaviwili’ ameiomba serikali iongeze nguvu kwenye mchezo wa masumbwi, ili utumike kuitangaza Tanzania.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Vifuaviwili alisema mabaondia wengi wanatamani kuitangaza nchi kimataifa lakini wanashindwa kutimiza ndoto zao kutokana na sapoti ndogo wanayopata kutoka serikali.

“Kazi yetu ni kubwa na ngumu, serikali imekuwa ikitupa sapoti lakini bado haitoshi tunaomba iongeze.

“Tunaona jinsi wanavyoipa sapoti timu ya Taifa, sasa na sisi tunahitaji ya namna hiyo ili tuzidi kuipepereusha vyema bendera yetu,” alisema.

“Naamini serikali yangu ni sikivu na itaunga mkono ili kuwasaidi mabondia hapa nchini,”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here