Mugabe kuzikwa nyumbani kwao

0
520

Harare, Zimbabwe

MWILI wa Rais  wa kwanza wa Zimbabwe, Robert Mugabe utazikwa nyumbani kwao, baada ya serikali kubadili msimamo wake wa awali kuhusu mazishi hayo.

Awali serikali ilitangaza kuwa Mugabe atazikwa katika makaburi ya mashujaa wa kitaifa, kauli ambayo kabla ya kukubaliwa ilipingwa na familia yake ikisema kuwa inakwenda kinyume na wosia wake.

Baada ya msimamo wa sasa, ibada ya mazishi Mugabe ambaye alifariki mapema mwezi huu akiwa na miaka 95 nchini Singapore, itafanyika katika mji mkuu wa Harare.

Baada ya ibada hiyo Mugabe atazikwa katika eneo la Zvimba, Taarifa kutoka ndani ya familia hiyo zinaeleza kuwa serikali ilibadili msimamo wake juzi Alhamisi.

Haikubainika kilichosababisha mipango ya awali ya mazishi ya Mugabe kubadilishwa.

Familia ya Mugabe ilikubali azikwe katika makaburi ya Heroes Acre baada ya makubaliano kufikiwa kuwa mnara wa makumbusho utajengwa kumuenzi kiongozi huyo wa kwanza wa Zimbabwe.

Katika taarifa iliochapishwa Alhamisi, Waziri wa Mawasiliano Nick Mangwana alisema mabadiliko hayo yanazingatia sera ya “kuheshimu uamuzi wa familia ya marehemu”.

Mugabe ambaye alifariki kwa ugonjwa wa saratani baada ya kifo chake familia yake ililamika hadharani kuwa haikushauriwa kuhusu mipango ya mazishi yake ya kitaifa.

Katika taarifa familia hiyo iliilaumu serikali kwa kutumia nguvu kupanga mazishi ya Mugabe katika makaburi ya mashujaa kinyume na “matakwa ya Mugabe”.

Taarifa hiyo aidha ilisema kuwa ombi lake la mwisho lilikua la mke wake , Grace Mugabe, kutoondoka kando ya jeneza lake hadi atakapozikwa.

Mugabe na familia yake inasemekana kughabishwa na jinsi alivyong’olewa madarakani na mshirika wake, wa zamani Rais Mnangagwa, miaka miwili iliyopita.

Hali hiyo ndiyo inayotajwa kuwa huenda imesababisha mvutano kuhusu mahali atakapozikwa.

Inaaminiwa kuwa wakati Mugabe akielekea kuchoka, Mama Taifa wa zamani Zimbabwe, Grace Mugabe, alikuwa amrithi mume wake jambo ambalo linatajwa kuwa nyuma ya mapinduzi ya kistaarabu ya kumwondoa madarakani.

Mugabe ndiye alikua Rais wa kwanza wa Zimbabwe baada ya nchi hiyo kupata uhuru 1980 na alitawala kwa miaka 37 hadi alipoondolewa madarakani kwa mapinduzi hayo ya kistaarabu mwaka 2017 na wadhifa wake kuchukuliwa na Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa.

Miaka ya awali ya uongozi wake, alisifiwa kwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya na elimu kwa waafrika walio wengi.

Lakini baadae utawala wake ulikumbwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi na ukandamizaji wa wapinzani wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here