27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Vifo lori la mafuta vyafikia 104

Aveline Kitomary -Dar es salaam

VIFO vya ajali ya lori la mafuta iliyotokea Agosti 10 mwaka huu eneo la Msavu mkoani Morogoro,imeendelea kuongezeka na kufikia 104,baada ya majeruhi wawili kati ya 13 waliokuwa wanapatiwa matibabu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kufariki dunia.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma MNH, Aminieli Aligaesha alisema Dar es Salaam jana waliofariki dunia ni Asha Ally Seleman (28) na Avelina Pastory Aman.

Alisema kati ya majeruhi 47 waliofikishwa hospitalini  hapo kupatiwa matibabu, tayari 36 wamefariki dunia.

 ” Majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea Morogoro ambao walikuwa wanapatiwa matibabu hospitalini hapa wanaendelea kupoteza maisha,baada ya Asha Ally Seleman (28) kupoteza maisha  Agosti 28,mwaka huu na Avelina Aman (30) kufariji Agosti 31.

 “Kuna mwili mmoja wa  Avelina upo chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri taratibu za kusafirishwa kwenda Morogoro kwa ajili ya mazishi,”alisema Aligaesha.

Alisemasasa majeruhi wamebaki 11 kati ya yao watano wako chumba cha uangalizi maalumu (ICU) na wengine sita wodi za kawaida.

 “Kati ya majeruhi 11 wanaoendelea kupata matibabua,watano wako vyumba vya ICU, sita wapo wodi 22 jengo la   Sewahaji,” alisema Aligaesha.

Wakati huo huo, miili ya marehemu watano wa ajali iliyotokea Kibiti mkoani Pwani ambayo inahusishwa lori la Kampuni ya Dangote na gari dogo kugongana,kisha kulipuka imehifadhiwa Muhimbili ikisubiri utambuzi wa vipimo vya vinasaba (DNA).

Aligaesha alisema miili hiyo, ilipokelewa Agosti 31,mwaka huu saa 5 asubuhi, huku ikiwa imeungua na kufanya iwe vigumu kutambulika.

“Miili ni ya watu wazima wanne na mtoto mmoja imeungua mno (beyond recognition), utambuzi wake ni mgumu.

“Tayari Hospitali ya Taifa Muhimbili imefanya uchunguzi (postmortem) na kuchukua sampuli kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha Forensic Pathology pamoja na Mkemia Mkuu wa Serikali ili kufanya uchunguzi zaidi,”alisema.

Alitoa wito kwa ndugu wa karibu na marehemu kujitokeza leo ili kuchukuliwa sampuli.

“Tunawaomba ndugu wa karibu  wa marehemu, hasa baba,mama na watoto wajitokeza kuanzia kesho (leo) saa 2 asubuhi ili wachukuliwE sampuli na Mkemia Mkuu wa Serikali,”alisema .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles