23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

AFRECO kuipa basi hospitali ya Mkapa

Mwandishi Wetu-Tokyo

TAASISI ya Association of African Economy and Development in Japan (AFRECO), imeahidi kuipatia Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Chuo Kikuu cha Dodoma basi ambalo ni hospitali kamili litakalotoa huduma za matibabu kwa Manispaa ya Dodoma, mikoa na wilaya zinazoizunguka mkoo huo.

Basi hilo litakapowasili nchini kutoka Japan, linatarajiwa kuwa mkombozi kwa wananchi waishio vijijini na maeneo ambayo hayana hospitali, kwani kila litakakokwenda kutoa huduma litakuwa na madaktari waliobobea katika utaalamu wa tiba mbalimbali, vifaa tiba, maabara pamoja na dawa.

Hayo yamebainishwa jana  na Rais wa   AFRECO,Tetsuro Yano wakati wa mazungumzo yake na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yaliyofanyika Yokohama nchini Japan.

 Yano alisema wameamua kuanza kutoa misaada na huduma zao  Tanzania, baada ya kufurahishwa na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali za kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Alisema anaamini siku moja Tanzania itakuwa nchi ya mfano Afrika Mashariki na Afrika yote kwa kutoa huduma bora za tiba, kwani itakuwa na vituo vingi vya afya na hospitali zenye uwezo wa kutibu magonjwa kama vile ya moyo na figo. Tayari wagonjwa kutoka nchi jirani wameanza kuja kutibiwa nchini.

Kwa upande wake, Majaliwa alisema mbali na kutoa basi ambalo litakuwa linatoa huduma za matibabu, pia taasisi hiyo itasaidia kupandisha hadhi Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Chuo Kikuu cha Dodoma kuwa shule kamili ya tiba.

Alisema hospitali hiyo, itapatiwa vifaa   mbalimbali vya tiba ambavyo vitaifanya kuwa shule bobezi   kwa utoaji,

Alisema wamekubaliana na AFRECO kuanzisha kitivo maalum cha uhandisi wa vifaa tiba ambacho kitafundisha uhandisi wa vifaa tiba ili nchi yetu iwe na watalaamu wa  kukarabati vifaa tiba pindi vinapoharibika badala kuvipeleka nje ya nchi au kuagiza wahandisi na watalaamu kutoka nje ya nchi kuja kuvitengeneza.

Naye Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma,  Mipango, Utawala na Fedha, Profesa Donald Mpanduji alisema wametia saini hati ya makubaliano kati ya  AFRECO na chuo hicho ambayo yanalenga kuboresha hospitali ya Chuo Kikuu cha Dodoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles