27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Vardy adai ilikuwa kazi rahisi kuibwaga Arsenal

Jamie Vardy
Jamie Vardy

LONDON, ENGLAND

MSHAMBULIAJI wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini England, Leicester City, Jamie Vardy, amedai kuwa ilikuwa kazi rahisi kuitolea nje klabu ya Arsenal katika kipindi cha usajili.

The Gunners walikuwa mbioni kumnasa mchezaji huyo wa timu ya taifa ya England na ilidaiwa kwamba tayari aliwasili jijini London kwa ajili ya kumalizana na klabu hiyo ya Arsenal, lakini dili hilo la pauni milioni 22 lilishindikana.

Vardy amedai kwamba, ilikuwa kazi rahisi kwamba kuitosa Arsenal na kubaki katika kikosi chake ambacho alikipa ubingwa wa Ligi Kuu.

“Nilikuwa nimekaa kwenye chumba cha hoteli mjini Chantilly kwa muda wa saa kadhaa bila ya kufanya jambo lolote, hapo ndipo kichwa changu na moyo ukaanza kuwaza juu ya maisha yangu ya soka kwa upande wa Arsenal na Leicester City.

“Akili yangu ikanituma nifanye maamuzi sahihi na si kujizungusha, lakini muda wote huo ni wazi kwamba moyo wangu na akili zangu zilikuwa zinaniambia kuwa baki Leicester City, nikaona bora nifanye maamuzi hayo ya kubaki katika klabu ambayo imenipa jina kubwa.

“Nilikuwa nawaza nini kinaweza kutokea nikisaini mkataba na klabu ya Arsenal na nini kitatokea kwa upande wa Leicester City nikiondoka, nikaona bora niendelee kubaki hapa.

“Naweza kusema kuwa ilikuwa kazi rahisi sana kufanya maamuzi ya kuiacha Arsenal na sasa naendelea vizuri na klabu hii na ninaamini nitaendelea kufanya makubwa zaidi msimu huu,” amesema Vardy.

Vardy mwenye umri wa miaka 29, amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuiunga mkono timu hiyo kwa ajili ya kuipa nguvu katika msimu huu mpya wa ligi na michuano mbalimbali Ulaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles