24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Uwanja Yanga wafikia pazuri

NA ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

KAMATI ya Ujenzi wa Uwanja wa Yanga, imekamilisha hatua ya pili ya kupata michoro, huku ikiwa mbioni kutangaza zabuni kwa ajili ya kuanza ujenzi.

Kamati hiyo inayoongozwa na Mhandisi, Bahari Mwaseba,juzi jioni ilikutana katika makao makuu ya klabu hiyo.

Hicho kilikuwakikoo cha tano ya cha kimkakati kwa ajili ya ujenzi wa uwanja katika eneo la Kigamboni, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana,Mhandisi

Mwaseba alisema kuwa katika kikao hicho, mbali ya kukamilisha michoro, pia kamati ilikabidhi ripoti ya bajeti itakayotumika katika ujenzi wa uwanja huo.

“Tumekamilisha jambo muhimu katika harakati za ujenzi wa uwanja wa Yanga, michoro ipo tayari na gharama za ujenzi kwa awamu ya kwanza.

Kinachofuata ni kutangaza tenda ili kutafuta mkandarasi, tukishampata tutawapelekea ripoti wananchi wenye timu yao ili wajue ni eneo lipi tunahitaji nguvu yao pamoja na mikakati ya ujenzi kwa ujumla ipo vipi,”alisema Mwasema 

Aliongeza:“ Matumaini yetu tutatetekeleza mradi huu kwa ushirikiano wa karibu na wadhamini wetu na muda ukifika watasema ni kwa mamna gani watashiriki katika hili,  kwa sababu huu ni mradi mkubwa wenye viwanja viwili, hosteli, bwawa la kuogelea na huduma nyingine za kijamii.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles