24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mtibwa yamuibua Mwenyekiti wa zamani Simba

ZAINAB IDDy-DAR ES SALAAM

SARE ya bao 1-1 iliyoipata Simba dhidi ya Mtibwa Sugar,imemuibua mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Swedy Mkwabi, ambaye amesema bado wana safari ndefu na ngumu katika kutimiza malengo ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Timu hizo ziliumana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Huo ulikuwa mchezo wa pili kwa Simba msimu huu, baada ya kuzindua kampeni zao kwa ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya timu mpya katika Ligi Kuu ya Ihefu ya mkoanji Mbeya, mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine.


Mkwabi ambaye alijiuzulu nafasi hiyo kwa  madai ya kutaka kujipa muda wa kutosha wa kushughulikia biashara zake, juzi alikuwa miongoni wa wanachama wa klabu hiyo waliojitokeza Uwanja wa Jamhuri kuishuhudia Simba ikiumana na Mtibwa. 

Akizungumza na MTANZANIA, Mkwabi alisema alama nne walizopitapa katika mechi za ugenini sio mbaya, lakini watatakiwa kupambana zaidi ili waweze kutimiza malengo yao ya kutwa taji tena.

“Mechi ya kwanza licha ya kupata alama tatu lakini wachezaji walikutana na upinzani mkubwa, na hata hii ya jana (juzi) bado unaona ni jinsi gani timu pinzani zinaikamia Simba.

“Inawezekana ni kwa sababu Simba tayari mabingwa au wapinzania nao wanataka kuonyesha umwamba wao,kwa hali hii kama yatafanyika makosa kidogo tu ndani ya uwanja, nje au kwa uongozi tutauweka rehani ubingwa wetu.

“Wachezaji wanapaswa kufahamu msimu huu wa ligi ni mgumu sana kwa Simba  hivyo wanatakiwa kujitoa katika hali zote ili tuweze kuyafikia malengo  yaliyowekwa,pia hata uongozi unapaswa kutoruhusu aina yoyote ya mpasuko ili kutowachanganya vijana wetu,”alisema Mkwabi.

Aliongeza:“Simba ina nafasi kubwa ya kutetea ubingwa msimu huu kwa sababu wachezaji wengi wameendelea kuwa pamoja, lakini hiyo haitoshi kujihakikishia hilo, iwapo kama hakutakuwa na uchezaji wa jasho na damu kwa ajili ya timu.”

Katika hatua nyingine, Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola alisema miundombinu isiyokidhi viwango ni sababu ya kikosi chao kukosa pointi dhidi ya Mtibwa.

“Inawezekana yakaonekana matokeo sio mazuri,kwa kuwa tumepata sare, lakini kwetu hatuna mtazaamo huo kwa sababu kupata lama nne ugenini katika viwanja kama vile ni kitu cha kushukuru pia.

“Sasa tunarejea nyumbani kucheza na Biashara United, bila shaka utakuwa mchezo mzuri kwetu na ndio utakaotupa ushindi wa idadi kubwa ya mabao kulingana na ‘pichi’ tunayokwenda kuitumia,”alisema Matola ambaye ni kiungo wa zamani wa Simba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles