24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wa dini wazungumzia miradi ya GGML, Serikali

NA MWANDISHI WETU

VIONGOZI wa kidini mkoani Geita wamefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa mkoani humo na kueleza kufurahishwa na usimamizi dhabiti miradi hiyo kwa maendeleo ya Tanzania.

Viongozi hao walifanya ziara hiyo ambayo imedhaminiwa na Kampuniya Geita Gold Mining Limited (GGML) pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita kwa lengo la kuona na kupata ufafanuzi wa miradi inayotekelezwa mkoani humo.

Akizungumzia ziara hiyo iliyofanywa jana, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel alisema ofisi yake inatambua mchango wa viongozi wa dini katika kutunza amani na umoja ndani ya jamii. 

“Huwezi kupata maendeleo katika jamii yoyote bila kuwa amani. Amani inayotupatia maendeleo katika nchi yetu na mkoa wetu wa Geita inalindwa na viongozi wa dini ambao siku zote wamekuwa na ushawishi kwa waumini wao kuhubiri amani,” alisema.

Aidha, Meneja Miradi inayofadhiliwa na GGML kupitia fedha za Wajibu wa Kampuni kwa Jamii (CSR), Moses Rusasa alisema katika ziara hiyo kuwa lengo la kampuni hiyo ni kuhakikisha jamii inayozunguka mgodi inafaidika.

“Tunatekeleza miradi mingi ndani ya Mkoa wa Geita kwa sababu mojawapo ya tunu inayoongoza Kampuniya GGML ni kufaidisha jamii inayotuzunguka. Katika ziara hii na viongozi wa dini, tumetembelea Soko la Dhahabu, Soko la Katundu pamoja na kituo cha uwekezaji (EPZA) miradi ambayo imefadhiliwa na Kampuni ya GGML kwa maendeleo ya watu wa Geita,” alisema  Rusasa.

Akitoa neno la shukrani wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Dini Mkoani Geita, Askofu Stephano Saguda alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa kuwatembeza katika ziara hiyo na kumpongeza kwa kazi nzuri ya kusimamia maendeleo katika Mkoa wa Geita.

“Tunampongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli kwa kuupatia Mkoa wa Geita kiongozi makini anayesimamia maendeleo. Nawapongeza pia Kampuni ya GGML kwa kushirikia na vyema na Serikali hususani Halmashauri za Geita na kutekeleza miradi mikubwa yenye gharama kubwa katika Mkoa wa Geita,” alisema Askofu Saguda.

Kwa miaka 10 iliyopita, GGML imewekeza Jumla ya Dola Milioni 25 kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani Geita na Tanzania kwa ujumla. Mkakati ni kutenga pia Dola Milioni 53 kwa ajili ya miaka 14 ijayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles