29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

UVCCM yazindua Tandale ya Kijani Dar

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umezindua tawi jipya katika Kata ya  Tandale Wilaya ya Kinondoni ‘Tandale ya Kijani’  ikiwa ni muendelezo wa kampeni yao ya Dar es Salaam ya kijani .

Uzinduzi huo ambao umeshafanyika katika Kata saba hadi sasa wilayani humo ukiwa umebeba kaulimbiu isemayo ‘Umeme umewaka Taa ya nini?’.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jana, Naibu Katibu Mkuu UVCCM Tanzania Bara na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa (NEC) Galila Wabanh’u aliwahimiza wanachama wenzake wa CCM kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa utaofanyika Oktoba mwaka huu Tandale ya kijani  ikawe chachu ya kuwachagua viongozi kwa kuzingatia kanuni, katiba na taratibu za chama hicho.

“Tukifanya hivyo, tutawapata viongozi wanaokubalika kwenye jamii na hivyo kutuhakikishia kushinda mapema,” alisema.

Aidha aliwaasa wanachama wenzake hususani vijana kuwa wenye kujiamini na chama hicho kinahitaji vijana  wenye ujasiri wa kuhoji na kupiga vita mambo ya hovyo yasiyoendana na maadili,  wala yasiyo na maslahi kwa nchi.

Akawataka kutokubali kushirikiana na watu au viongozi wanaotoa rushwa kutafuta kuungwa mkono au wanaofanya siasa za kukigawa chama kuwala wasiwavumilie kwani umoja na mshikamano ndio nguvu ya CCM kwenye chaguzi.

“Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa nchi yetu  si muumini wa siasa za makundi wala rushwa, tumuunge mkono kwa kuzikataa siasa za makundi na rushwa ndani ya chama chetu kwa nguvu zetu zote kwani hivi vyote ni sumu ya umoja na mshikamano wetu,” alisisitiza Galila.

Wabanh’u aliwataka vijana kuacha kulalamika na baadala yake wawe wabunifu na kuchangamkia fursa za mafunzo yanayoweza kuwapa ujuzi wa kujiajiri ambapo alitolea mfano ujasiriamali na kuanzisha miradi ya kiuchumi ikiwamo uundaji wa vikundi ili iwe rahisi kupata mikopo au misaada mingine ili waweze kujikwamua na umaskini.

Katika kuunga mkono juhudi za vijana Wabanh’u aliahidi kutoa Sh milioni moja kwa saccos ya vijana Kata ya Tandale.

Aidha aliwataka vijana wa CCM kuzisemea changamoto zinazoyakabili makundi ya machinga, bodaboda, bajaji, mama lishe, wanafanyakazi viwandani, wavuvi, mafundi gereji na makundi mengine kama hayo kwani huo ni wajibu wa msingi wa UVCCM.

“Hili liendane na kuwaondolea wananchi kero ambapo aliitaka CCM Kinondoni kutokuwa na huruma wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya chama hicho,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles