24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Jeshi la zimamoto laagizwa ukaguzi wa majengo yote

ALLAN VICENT – TABORA

Askari wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji nchini wameagizwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika majengo ya umma na ya wananchi na kuhakikisha yanafungwa ving’amuzi vya moto na vifaa vya kuuzimia ili kuepusha madhara na uharibifu moto unapotokea.


Agizo hilo limetolewa leo Juni 17, na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Thobias Andengenye alipokutana na waandishi wa habari mkoani hapa akiwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji majukumu ya jeshi hilo.


Andengenye  amewataka askari wa jeshi hilo kuhakikisha wanakagua majengo yote katika mkoa huo ili kuangalia kama wahusika wanazingatia matakwa ya kikanuni na kisheria ya kuzuia majanga ya moto katika majengo hayo.

Ameitaka jamii kutambua umuhimu wa kuwa na ving’amuzi vya majanga ya moto katika majengo yao na vifaa vya kuuzimia yao ambavyo havina gharama kubwa ili kufanikisha mapambano dhidi ya majanga hayo.

“Askari wa Jeshi la zimamoto elimisheni jamii kuhusu majanga ya moto, hamasisheni wanafunzi na jamii kwa ujumla kuanzisha klabu za kuzuia, kuzima na kuokoa wahanga wa majanga ya moto’, amesema.

Aidha ndengenye amewataka wakurugenzi watendaji wa halmashauri zote nchini kulipa kipaumbele suala la kutenga maeneo ya kujenga vituo vya zima moto na uokoaji katika halmashauri zao ili kuongeza ulinzi wa mali na miundombinu iliyopo dhidi ya ajali za moto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles