22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Utoroshaji mawe ya dhahabu migodini waanza kudhibitiwa

Na Derick Milton, Simiyu

Ofisi ya Madini Mkoa wa Simiyu imeanza oparesheni inayolenga kudhibiti vitendo vya utoroshaji wa mawe ya madini ya dhahabu katika migodi ya Bulumbaka na Lubaga iliyoko Halmashuari ya Wilaya ya Bariadi Mkoani humo.

Hatua hiyo ya Ofisi ya madini, inakuja baada ya kuwepo kwa vitendo vya vilivyokidhiri vya utoroshaji wa madini hasa mawe, ambavyo ufanywa na wachimbaji kwa kushirikiana na wanunuzi wa wadogo na wa kati wa madini.

Hayo yamebainishwa leo na Kaimu Ofisa Madini Mkoa, Mhandisi Joseph Kumburu, wakati wa semina kwa wanunuzi wa kati na wadogo wa madini, iliyolenga kujiepusha na vitendo vya utoroshaji wa madini na ukwepaji wa kodi na mirahaba ya serikali.

Mhandisi Kumburu amesema kuwa licha ya vitendo vya utoroshaji wa madini yenye kudhibitiwa kwa kiwango kikubwa, tatizo lilibaki kwenye utoroshaji wa mawe yenye madini kupitia njia za udanganyifu.

“Kilichokuwa kinafanyika uko nyuma mifuko ya mawe ambayo yametoka kwenye duara na tunajua kuwa yana dhamani, wao walikuwa wanatumia njia kuwa mifuko hiyo ni ya freshio, la kambi, mkaguzi, usafi, au mafero.

“Kilichokuwa kinafanyika kabla ya mnada walikuwa wanatoa baadhi ya mifuko yenye mawe kuipeleka kwenye maeneo hayo kutokana na kuwepo wa msamaha na wao walikuwa wanatumia njia hiyo kukwepa kodi,” amesema Mhandisi Kumburu.

Amesema kuwa ofisi yake iliamua kufanya uchunguzi na kubaini utoroshwaji mkubwa wa mawe kupitia visingizio hivyo vinavyofanywa na wanunuzi pamoja na wachimbaji ambapo wamefanikiwa kuvidhibiti.

“Baada ya kugundua hilo tumedhibiti mianya hiyo, tumegundua kuwa utoroshaji ulikuwa mkubwa, kwa sasa tumeelekeza hatua ya kwanza baada ya mifuko kukusanywa ni mnada na siyo mgao kama ilivyokuwa,” ameongeza.

Katika semina hiyo imeshirikisha vyombo vya ulinzi na usalama (Polisi na Takukuru) ambapo vyombo hivyo vimewataka wanunuzi hao kuacha mara moja na kutojihusisha na wizi wa madini.

Kaimu kamanda wa polisi Wilaya ya Bariadi, Mpamba Suleiman amesema kuwa tangu kuanza kuchimbwa kwa madini katika wilaya hiyo jumla ya kesi nane zimeripotiwa kwenye jeshi hilo.

“Mpaka sasa tunazo kesi nane, nyingine uchunguzi umekamilika na wahusika wapo mahakamani na nyingine tunaendelea kuchunguza, niwaombe wanunuzi acheni kujihusisha na vitendo hivi fuateni sheria za madini,” amesema Mpamba.

Naye, Mkuu wa Uchunguzi taasisi ya Kuzia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa Aquilinus Shiduki aliwataka wanunuzi hao kuhakikisha wanafuata taratibu zote zinazotakiwa kwenye kazi yao na kuepuka vitendo vya rushwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles