Utata mtoto wa Diamond, Tanasha amwaga uthibisho

0
1780
Diamond Platnumz akimbeba mwanawe

SWAGGAZ RIPOTA

KATIKA kuadhimisha miaka 30 ya kuzaliwa kwa staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, yeye na mpenzi wake raia wa Kenya wametangaza kupata mtoto wao wa kwanza  wa kiume aliyezaliwa hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam Jumatano wiki hii.

Kama ilivyo kawaida kwa staa huyo na familia yake kugonga vichwa vya habari za burudani basi mtoto kulizaliwa siku moja na baba yake kumezua gumzo tena na kuwagawa mashabiki  ambao wengine wamewapongeza na wengine wakidai kuwa kapo hiyo imedanganya.

Tena wametangaza uongo kwani mtoto alishazaliwa kitambo ila familia hiyo ilitaka kutengeneza kiki ili ionekane baba (Diamond Platnumz) na mtoto wake wamezaliwa tarehe moja.

Mashaka hayo yanakuja baada ya siku kadhaa zilizopita kuzuka kwa tetesi kuwa Tanasha ameshajifungua licha ya Diamond na Tanasha kutozungumza chochote ila watu wao wa karibu kama vile baba yake Diamond aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akisema Tanasha amejifungua.

Siyo hivyo tu kumekuwa na ishara mbalimbali ambazo familia ya staa huyo imekuwa ikizionyesha kabla ya  wawili hao kutangaza kupata mtoto, siku ambayo Diamond pia amezaliwa jambo ambalo linaonekana kama ni kiki.

Katika kuonyesha mtoto wao ni kweli amezaliwa siku moja na baba yake, Diamond Platnumz na familia yake walikata keki ya ‘birthday’ katika moja ya wodi la hospitali ya Aga Khana ambayo Tanasha alijifungulia.

Hali kadhalika, Tanasha ambaye ni raia wa Kenya hakukaa kimya baada ya tetesi hizo kushika kasi na akaamua kujibu kupitia mtandao wa Instagram kuwa ni kweli amejifungua siku ambayo mpenzi wake (Diamond) alizaliwa.

Mrembo huyo alitumia Insta Stories kuweka kibandiko maalum cha hospitali ya Aga Khan kinachoonyesha maeelezo yote muhimu ya kuzaliwa mtoto wake huyo wa kwanza kama vile tarehe ambayo ni Oktoba 2, mwaka huu na namba ya kuzaliwa ni 158-03-1.

Akizungumzia  tukio la kujifungua Tanasha anasema: “Nimekaa leba kwa saa 17 na ujauzito wangu umedumu kwa wiki 42, nimejifungua kwa njia ya kawaida, yote hayo yana maana kubwa kwangu sasa mimi ni mama wa mtoto mzuri wa kiume anayeshea ‘birthday’ na mpenzi wangu (Diamond).”

Mastaa na watu mbalimbali wameipongeza kapo hiyo kwa kupata mtoto wao wa kwanza huku  kwa Diamond akiwa ni mtoto wake wa tano. Mondi  amewahi kusema katika kipindi cha Kaa Hapo cha TBC, kuwa alikuwa na mtoto mkubwa jijini Mwanza kabla hajampata Tiffah na Nillan kwa Zari The Boss Lady na Daylan kwa Hamisa Mobetto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here