31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

‘Usonji bado changamoto kubwa nchini’

 

Mkuu wa kitengo watu wenye tatizo la ugonjwa wa Usonji, Dk. Stella Rwezaula (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuzinduzi wa warsha maalumu ya uelewa kuhusu tatizo la Usonji nchini Dar es Salaam jana. Nayefuatia ni Mkurugenzi wa kituo cha Afya cha Lotus Dialla Kassam  pamoja na mtaalamu wa mambo ya usonji dunia, Kevin Baskerville, kutoka Leicestershire nchini Uingereza. Na Mpigapicha Wetu
Mkuu wa kitengo watu wenye tatizo la ugonjwa wa Usonji, Dk. Stella Rwezaula (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuzinduzi wa warsha maalumu ya uelewa kuhusu tatizo la Usonji nchini Dar es Salaam jana. Nayefuatia ni Mkurugenzi wa kituo cha Afya cha Lotus Dialla Kassam pamoja na mtaalamu wa mambo ya usonji dunia, Kevin Baskerville, kutoka Leicestershire nchini Uingereza. Na Mpigapicha Wetu

Na Hadia Khamis-DAR ES SALAAM

TANZANIA bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya kukabiliana na ugonjwa wa usonji ambao wengi hawautibu kutokana na kutoelewa dalili zake, imefahamika.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Usonji Kitaifa (NAPA-T), Dk. Stella Rwezaura, alisema hadi sasa bado wazazi na walimu hawajaweza kufahamu mtoto mwenye tatizo la usonji.

“Dalili za usonji bado hazijafahamika vizuri kwa wazazi na walimu nchini, hivi wanashindwa kuutibu ugonjwa huu au kupata msaada wa kitaalamu kwani ni ugonjwa ambao una mambo mengi yanayoathiri namna mtu anavyowasiliana na mara nyingi huwa na tabia ya kufanya vitu kwa kurudia rudia bila kukusudia,” alisema.

Alisema kwa mwaka huu, Kituo cha Afya cha Lotus (LHC), ambacho si cha Serikali na kinafanya kazi za kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu, kimeifadhili NAPA-T kufanya warsha inayolenga kutoa elimu kuhusu usonji na itawaleta pamoja washiriki takribani 100 kutoka sekta binafsi na za kiserikali.

“Huu ni moja ya mkakati wa LHC kutoa elimu katika jamii na kuwaleta pamoja watoto na wazazi wenye mahitaji maalumu,” alisema.

Alisema mojawapo ya kazi za NAPA-T kwa kushirikiana na LHC, ni kutoa elimu na mafunzo ya kutosha kuhusu ugonjwa huu ikiwamo katika Serikali na mitaa na Serikali kuu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa LHC, Dialla Kassam, alisema wanajivunia kufanya kazi na NAPA-T na kumshukuru mfadhili kutoka Uingereza, Kevin Baskerville, ambaye ni mtaalamu wa usonji kwa msaada wake kwani amekuwa akija Tanzania mara kwa mara kutoa mafunzo na elimu kuhusu ugonjwa huo.

“Kupitia warsha iliyoandaliwa na LHC mwaka jana, International School of Tanganyika (IST) ilishirikiana na  Shule ya Msimbazi Mseto ya watoto wenye mahitaji maalumu, na watoto wa Msimbazi Mseto sasa wanaruhusiwa kwenda IST kuogelea mara moja kwa wiki,” alisema.

Alisema LHC pia imekuwa ikitoa msaada kwa shule ya watu wenye usonji ya Mbuyuni kwa kupitia wataalamu wa kujitolea kutoka pembe zote za dunia na kusimamiwa na LHC ambayo pia hutoa rasilimali za elimu kwa shule hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,586FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles