32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

JPM amtumbua mkurugenzi aliyemtishia trafiki

pombe-620x308Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

SIKU moja baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga kufikishwa mahakamani kwa kutishia kumuua askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Rais Dk. John Magufuli ametangaza kutengua uteuzi wake.

Mkurugenzi huyo, Emmanuel Mkumbo (41) juzi alipandishwa kizimbani mkoani Morogoro na kukana mashtaka yote yanayomkabili na kuachiwa kwa dhamana.

Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, ilieleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkumbo kuanzia jana.

“Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Emmanuel Mkumbo kuanzia leo (jana) Oktoba 18, 2016. Uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga atakayejaza nafasi ya Emmanuel Mkumbo utafanywa baadaye,” ilieleza taarifa hiyo.

Mkumbo alipandishwa kizimbani juzi na kusomewa mashtaka kadhaa, likiwamo la ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani, lenye makosa mengine matano.

Inadaiwa siku hiyo huko Mbuyuni Mkambarani, mkoani Morogoro, mshtakiwa aliendesha gari namba T 845 CTJ aina ya Prado bila kuwa na leseni, bima, mwendokasi wa spidi 85 badala ya 50 zilizoruhusiwa eneo hilo.

Mbali na hilo, pia alidaiwa kukataa kupeleka gari kituo cha polisi kilicho jirani kama alivyoamriwa na askari WP 5392 Sajenti Anna na kosa jingine ni kusimamisha gari katikati ya barabara kwa uzembe, bila uangalifu na kutozingatia watumiaji wengine wa barabara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles