24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Usimwingize mwanao kwenye migogoro ya mahusiano

Ma CHRISTIAN BWAYA

MIGOGORO katika mahusiano ya ndoa ni jambo lisiloepukika. Hakujawahi kutokea watu wawili wenye vichwa tofauti wakaafikiana kwa kila jambo.

Kutofautiana kupo lakini tunafahamu kuwa hatua madhubuti zisipochukuliwa mapema kuondoa tofauti hizi ndoa in- aweza kukumbwa na tufani.

Inapofikia hatua hiyo wanandoa wanaweza kujikuta wakilazimika kuwahusisha watu wengine katika matatizo yao kwa sababu kadhaa.

Mosi, ni kuwasaidia kutatua mgogoro uliopo. Mmojawapo anapoomba msaada wa ndugu na jamaa wengine kwa mfano, analenga kupata msaada wa mawazo yatakayochangia kutatua changamoto zilizojitokeza.

Hata hivyo, si mara zote mwaliko huo wa watu wengine hulenga kutatua matatizo, wakati mwingine nia ya kuwaambia wengine huwa ni kutafuta huruma. Kwamba anapowaambia watu hali halisi kimsingi halengi kupata suluhu ya mgogoro unaoendelea ndani ya ndoa bali kutafuta faraja ya kisaikolojia kuwa anaonewa.

Katika mazingira ambayo ndoa iko kwenye mgogoro kwa sababu yoyote ile ni rahisi kwa wazazi kufikia hatua ya kuwa- husisha watoto wao kwenye matatizo yao.

Ninaomba kukushawishi kuwa jaribio lolote la kuwahu- sisha watoto na matatizo yenu si busara na inaweza kuleta mtafaruku mkubwa zaidi.

Jambo la kuzingatia ni kwamba changamoto yoyote mnayo- kumbana nayo kama wanandoa inawahusu ninyi wawili.

Matatizo yenu hayawahusu watoto wenu ingawa ni kweli unaweza kujaribiwa kutafuta huruma ya watoto ukweli ni kwamba kufanya hivyo ni kukosa ukomavu.

Katika mipaka ya makala haya mtoto ni mtu anayeendelea kukua kiufahamu na kimwili na anayetegemea msaada wa wazazi akiishi chini ya mamlaka yao.

Kuwaingiza watoto kwenye mgogoro kunaweza kutafsiriwa kama kuwapa watoto taarifa zisizo za lazima kuhusu mgogoro wenu kwa lengo la kuwafanya wajue nani ni mkosaji na yupi hana hatia.

Mfano, baba anapowajulisha watoto kuwa anaachana na mama yao hiyo haimaanishi kuwa anawaingiza watoto kwe- nye mgogoro, lakini anapowapa watoto maelezo ya kina ya kiini na historia ya mgogoro ili kuwafanya waelewe nani amefanya nini kumwonea nani, hapo tunasema anawaangiza watoto kwenye mgogoro usiowahusu.

Unaweza kuwapa taarifa hizi kwa lengo jema la kuwaelewesha kwa nini mnaachana lakini akili ya mtoto ikajenga msimamo dhidi ya mzazi mmojawapo.

Hatari kubwa ya kufanya hivi ni kuwafanya watoto wachukue upande.

Hali hii inaweza kuonekana kuwa jambo dogo lakini ikawa na athari kwa maisha ya mtoto kwa mfano, kwa kugundua kosa la mmoja wenu mtoto anaweza kujenga chuki na kisasi kitakachoathiri maamuzi yake ya ndoa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles