24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Urais wamchanganya Donald Trump

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS Donald Trump bado hajatulia, inaonekana matokeo ya urais badi yanamchanganya na sasa ameamua kumfukuza Waziri wa Ulinzi, Mark Esper na kuwazuia wafanyakazi wa Ikulu kutoa ushirikiano kwa Rais Mteule, Joe Biden.

Pamoja naye, viongozi katika utawala wa Rais Trump umepuzilia mbali matokeo ya uchaguzi, ambapo baadhi ya wanachama wa Republican, pamoja na kiongozi wa wengi katika Baraza la Seneti, Mitch McConnell, wameunga mkono juhudi zake kupinga matokeo ya uchaguzi na ni wachache pekee waounga mkono ushindi wa Biden.

Muendelezo wa matukio hayo unatia shaka iwapo taifa hilo litashuhudia mabadiliko ya uongozi kwa mustakabali wa amani na utaratibu kama ilivyokuwa katika miaka iliyopita hatua ambayo imekita mizizi katika kuimarisha Demokrasia yake ya muda mrefu. 

Mfumo wa wajumbe wa uchaguzi umeratibiwa kutoa matokeo rasmi ya ushindi wa Biden Desemba 14 na mwanademokrasia huyo ataapishwa kuingia ofisini mwishoni mwa Januari 20, 2021.

Mwanasheria Mkuu chini ya utawala wa Trump, William Barr ameagiza uchuguzi

Bada ya kuidhinisha mawakili kufanya uchunguzi kuhusu madai ya wizi wa kura na ulaghai katika uchaguzi, ingawa hakuna visa vyovyote vilivyoripotiwa kuhusu tatizo hilo katika uchaguzi wa 2020.

Maofisa wa uchaguzi kutoka vyama vyote vya kisiasa pamoja na waangalizi wa kimataifa walisema  upigaji kura ulikwenda vizuri na hakukuwa na kasoro.

Biden tayari ameanza mipango ya kujenga utawala wake na kuandaa timu ya wataalam kukabili janga linalozidi kuongezeka la corona, lakini wanaopaswa kutoa mwelekeo wa kuanza rasmi kwa zoezi hilo wamekwama kutokana amri ya rais Trump. 

Huku rais Trump akiendelea kuwachukulia hatua wanaokaidi amri yake, Seneta Chuck Schumer wa Republican alisema hatua ya Republican kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi ni hatari sana na ni sumu kali kwa demokrasia ya Marekani.

Republican wamekuwa wakisita kumshinikiza Trump kwenda kukubali ushindi wa Biden, wakijua ingemkasirisha na kuvuruga msingi wa uhusiano wao wa Trump.

Wengi pia hawakuwa wakimuhimiza Trump kuhusu madai ya kuwepo udanganyifu katika uchaguzi kwa wakiashiria kuwa madai hayo hayakuwa na msingi.

Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Utawala katika Ikulu ya Marekani, Emily Murphy aliyeteuliwa na Trump hajaanza mchakato wa kuelekeza utawala mpya wala hajatoa muongozo ni lini ataanza mchakato huo.

Ukosefu huo wa ufafanuzi unachochea maswali ikiwa Trump anatumia muda wake mwingi uliobaki ofisini kumzuia Biden kuunda serikali yake. 

Biden hadi sasa kwa kiasi kikubwa amekuwa akimpuuza Trump na badala yake kumuomba washirikiane.

ITAKUWAJE  IWAPO ATAKATAA KUONDOKA?

Iwapo Trump atakataa kabisa kutoka madarakani, huenda kukawa na ulazima wa kuangazia uaminifu wa wanajeshi kwa rais.

Baadhi ya wataalam ameeleza kuwa iwapo kuna uwezekano wa Trump kujaribu kutumia vikosi vya jeshi kusalia madarakani kinyume na sheria.

“Kwa rais kutumia vibaya madaraka kwa kuamua kusalia madarakani baada ya kupoteza uchaguzi, itakuwa vigumu na pia ni hali ambayo itakuwa inakwenda kinyume na kile ambacho kimekuwa kikizoeleka,” Profesa Dakota Rudesill, mtaalamu wa sera na masuala ya usalama wa taifa mwenye kuhusishwa na chuo kikuu cha Ohio Marekani aliiambia BBC.

“Itakuwa na athari mbaya kwa taifa hilo, kuanzia kanuni za msingi za uhusiano wa raia na jeshi na matarajio ya kidunia katika suala la demokrasia,” alionya.

Hata hivyo, aliweka wazi katika maoni yake kuwa, matukio yanayoweza kutoke ikiwa Trump atang’ang’ania kusalia madarakani kama ataungwa mkono na vikosi vya usalama.

“Wanajeshi walikula kiapo kutekeleza katiba kwa uaminifu na wala sio kuwa muaminifu kwa mwanasiasa aliye madarakani. Na afisa wa juu zaidi jeshini, Jenerali Mark Milley, mwenyekiti wa kamati ya wakuu wa wafanyakazi wote, amesema mara kadhaa kwamba jeshi halitajihusisha na chochote na uchaguzi huu,” alieleza.

Profesa Rudesill hayuko peke yake katika kuangazia kinachoweza kutokea, Keisha Blaine ni profesa wa Chuo Kikuu cha Pittsburgh na mtaalamu wa masuala ya maandamano.

“Ukweli wa kwamba imefika wakati ni lazima tujiulize ikiwa jeshi linaweza kuingilia uchaguzi kunaelezea mengi kuhusu hali ta kusikitisha inayokumba nchi yetu,” aliiambia BBC.

Miaka minne iliyopita, raia wengi wa Marekani hawakuwa na wasiwasi kuhusu hili. Lakini baada ya kumuona Trump akipeleka maofisa polisi na jeshi wa serikali kuu wakati wa maandamano huko Portland na Washington miezi ya hivi karibuni, sasa suala hili limezua wasiwasi. 

“Sioni kama hili linaweza kutokea lakini hatuwezi kuliondoa kabisa katika orodha ya yanayoweza kutokea hasa ukizingatia kilichotokea mwaka huu,” aliongeza.

Katika maandamano yaliyodai kupinga ubaguzi katika ya mwaka, Trump aliamua kupeleka wanajeshi kukabiliana na waandamanaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles