25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Biden aendelea na mipango ya kuunda serikali

Rais mteule wa Marekani Joe Biden anaendelea na mchakato wa kuujenga utawala wake, huku rais aliyeshindwa katika uchaguzi uliopita, Donald Trump akiendelea kuwasilisha mkururo wa kesi mahakamani.

Joe Biden anapanga kukutana leo Jumatano na kikundi cha washauri wake, ambao wanamsaidia kuweka msingi wa utawala mpya, na kumuandaa kula kiapo cha kuchukua madaraka aifikapo Januari 20 mwakani.

Miongoni mwa washauri hao ni wataalamu wa masuala ya kibenki na kifedha, wanaotoka chama chake cha Democratic pamoja na wale wenye mrengo usio wa kihafidhina, akinuia kuakisi mjadala unaoendelea ndani ya chama hicho juu ya namna ya kushughulikia changamoto za mabadiliko ya tabianchi na pengo kubwa kati ya matajiri na maskini.

Rais huyo mteule anawatumia watu waliopangilia sheria kali za kimazingira wakati wa utawala wa Rais Barack Obama.

Licha ya Rais Trump na maafisa wengi wa chama cha Republican kuendelea kukaidi kuyakubali matokeo ya uchaguzi wa Novemba 3, uchunguzi wa maoni ya raia uliofanywa na shirika la habari la Reuters kwa ushirikiano na shirika la utafiti la Ipsos, na ambao ripoti yake ilichapishwa jana Jumanne, umeonyesha kuwa asilimia 80 ya Wamarekani, wakiwemo nusu ya Warepublican, wanamkubali Biden kama mshindi halali. Kuendelea kupinga matokeo ni sumu kwa Demokrasia

US Präsidentschaftskandidat Mitt Rommey (picture-alliance/dpa/T. Smart)
Seneta wa Republican Mitt Romney

Mmoja wa Warepublican hao ni seneta Mitt Romney, ambaye amesema kuendelea kupinga matokeo ni doa kwenye sura ya Marekani.

”Sielewi ninapowasikia watu wanaosema uchaguzi ulikuwa na mizengwe na wizi. Kwa maoni yangu, hilo sio sahihi, na pili, ni hatari katika mchakato wa uhuru, kwa sababu macho yote ya dunia yanaitazama Marekani, kuangalia jinsi tunavyoushughulikia uchaguzi huu.” amesema Seneta Mitt Romney.

Kwa upande mwingine, Rais Donald Trump anaendeleza mchakato wake wa kimahakama, akishikilia madai yake ya udanganyifu katika uchaguzi alioupoteza, bila hata hivyo kuambatanisha malalamiko yake na ushahidi ulio bayana.

Tayari majaji wamekwiyatupilia mbali malalamiko ya Trump katika majimbo ya Michigan na Georgia, na wataalamu wa sheria wanasema mashitaka yake yana nafasi finyu ya kuweza kubadilsha matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyompa ushindi Biden.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles