26.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Upungufu wa maji jijini Mwanza waendelea kuwa mwiba

*Rc Malima atoa maagizo kwa mamlaka zinazohusi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Hali ya upatikanaji wa maji katika jiji la Mwanza ambao kwa sasa yanapatikana kwa mgao unaendelea kuwatesa wananchi huku viongozi wakitoa maagizo mbalimbali kwa mamlaka zinazohusika  kuhakikisha zinatatua changamoto hiyo.

Mkurugenzi Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira kutoka Mwauwasa  Mhandisi Salim Lossindilo akijibu hoja kwenye cha kujadili namna ya kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji mkoani Mwanza.

Hali hiyo ilimlazimu Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango akiwa mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi Septemba 14, 2022 baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa chanzo cha tiba ya maji Butimba kinachojengwa katika wilaya ya Nyamagana kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 48 za maji kwa siku na kuwanufaisha wakazi 450,000 kuiagiza Wizara ya Maji kuhakikisha unakamilika kabla ya Desemba 25, mwaka huu badala ya Februari 2023.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana ambaye baada ya wananchi kutoa kero zake kwake  alitoa maagizo kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (Mwauwasa) ambao wanasimamia mradi huo wa butimba kuhakikisha unakamilika mapema ili kuondoa kero hiyo kwa wananchi.

Ili kuhakikisha maagizo ya viongozi hao wa kitaifa yanafanyiwa kazi Mkuu wa Mkoa huo Adam Malima  Oktoba 25 alikutana na mamlaka zinazohusika kusimamia maendeleo ya sekta ya maji mkoani humo na kuziagiza kushughulikia  changamoto ya upungufu wa maji ili kuondoa kero hiyo kwa wananchi.

Meneja wa Ruwasa Mkoa  wa Mwanza Mhandisi Exaud Humbo akiwasilisha mada ya hali ya upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

Taasisi ambazo Malima alikutana nazo ni Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (Mwauwasa), Mamlaka ya maji mji wa Sengerema (Seuwasa ) na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa).

Malima alisema anatambua kwamba kwa makadirio hadi mwishoni mwa mwaka 2021 mahitaji ya maji katika mkoa huo ni lita milioni 160 kwa siku, ambapo chanzo kilichopo cha Capripoint kinazalisha lita milioni 90 hivyo upungufu  uliopo ni lita milioni 70 kwa siku ambao unasababisha Mwauwasa kutoa huduma hiyo kwa mgao lakini ni wajibu wao kuhakikisha wanatafuta namna ya kutatua  changmoto hiyo pia alisisitiza mradi wa butimba ukamilike kwa wakati.

“Vievile nataka ufanyike utafiti wa kina utakaosaidia kubaini hali ya upatikanaji wa maji ili huduma hiyo itolewe kwa usawa maana haipendezi eneo hili wanapata maji wakati wote halafu jingine zinapita wiki mbili hawajapata maji sambamba na hilo nataka umakini na ufanisi katika utekelezaji wa miradi ili kuondoa upotevu wa Maji uliofikia hadi asilimia 32 kwenye mradi mkubwa wa chanzo cha Kapripoint wenye uwezo wa kuzalisha lita Milioni 90.

Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Maji  Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara hiyo Mwajuma Waziri ambaye aliambatana na Mkurugenzi wa Mwauwasa Mhandisi Leonard Msenyele, wakandarasi na wafadhili wa mradi wa chanzo cha tiba ya maji Butimba ambao wako mkoani humo kikazi alisema wanaendelea kufanyia kazi agizo la Makamu wa Rais Dk Philip Mpango ili mradi huo ukamilike Desemba.

“Pia tunaendelea kufanya mazungumzo na wafadhili wetu ambao ni Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya(EIB) watupe fedha ili tuendelee kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo ya pembezoni mwa jiji la Mwanza lengo la serikali ni kuwahudumia wananchi,” amesema Malima.

Mkurugenzi Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira kutoka Mwauwasa  Mhandisi Salim Lossindilo akijibu hoja hizo alimwambia Malima kwamba sababu za kuwepo mgao wa maji ni  uchakavu wa mitambo ambao unakadiriwa kuhitaji Sh  bilioni tatu lakini wanaendelea na jitihada za kupata pampu zitakazosaidia kuongeza nguvu kwenye vituo vya usambazaji vya Mabatini, Kona ya Bwiru na Nyegezi ili wananchi wanaoishi pembezoni wapate maji ya kutosha.

“Tatizo la Mji wa Mwanza upo kama bakuli kijografia, yaani usambazaji wa maji unakua mgumu sana kwa wananchi wanaoishi pembezoni na kwenye maeneo ya miinuko, hali hii tutaiondoa kwa kuboresha miundombinu yetu ili iwe imara zaidi wakati wote tofauti na hivyo wakazi wanaoishi kwenye maeneo tambarare na chini watanufaika zaidi.

“Tukifanya ukarabati tutaweza kujaza matanki yaliyopo pembezoni kama la Nyashana ambalo kwa  sasa linajaa kwa asilimia 50 tu ila tutakapopata mitambo huduma ya maji kwa wananchi wanaoishi kwenye maeneo yenye miinuko itaimarika kwani uzalishaji na usambazaji utaongezeka,”amefafanua Mhandisi Lussindilo.

Meneja wa Ruwasa Mkoa  wa Mwanza Mhandisi Exaud Humbo alisema kwa mwaka wa fedha uliopita  2021/2022  wametekeleza miradi  yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 112 lakini msamaha wa kodi ni miongoni mwa changamoto walizonazo hali hiyo inasababisha miradi mingi kuchelewa kuanza taratibu za manunuzi.

“Kati ya miradi 29 ni miradi sita tu imepata msamaha lakini pia baadhi ya wakandarasi wanazembea kufanya kazi hao tumeamua kutoendelea nao lengo letu ni kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili iweze kuwanufaisha wananchi,”alisema Humbo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles