26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

RC Malima aahidi neema timu za Mwanza

*Atoa Sh milioni 20 kwa ajili ya kuziwezesha zifike ligi kuu Tanzania Bara

Na Clara Matimo, Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima ameahidi kuzisaidia timu za Mwanza zinazoshiriki ligi ya championiship kifedha na ushauri ili ziweze kushiriki ligi kuu Tanzania baramsimu wa 2023/24.

Malima ametoa ahadi hiyo Oktoba 25, 2022 alipokuwa akizungumza na wadau wa soka mkoani humo wamiwemo viongozi wa timu za Gwambina FC, Copco Veteran FC na Pamba FC zinazoshiriki ligi ya championship ambapo aliahidi kutoa kiasi cha Shmilioni 20 ikiwa ni mwanzo wa kuweka mikakati ya ushindi kwa timu hizo.

Amesema malengo na ndoto yake  ni kupata timu kutoka mkoani humo itakayocheza ligi kuu mwaka kesho lakini mpira hauchezwi bila pesa ambapo aliwapa wiki moja viongozi wa timu hizo wakahamasishane kwenye michango maana ili kufanikiwa wanahitaji kuwa na dhamira ya dhati kwenye soka na kujitoa kwa hali na mali pia aliwaasa kutodharau fedha yoyote itakayotolewa na wanachama hata kama ni Sh 5,000.

 “Kila mara nasema Mwanza bila kuwa na timu inayoshiriki ligi kuu hatuheshimiani hapa mjini, kitendo cha watu kutoka mkoani  Kagera au Geita ili kutupa starehe sisi ya kuona mpira hapa ni jambo la fedheha sana mimi fedha hizo ni mwanzo tu yawezekana tukikutana wiki ijayo nikawa nimepata zaidi maana naendelea  kuwachangisha marafiki zangu wengine lakini bila kuwa na dhamira ya dhati hatuwezi kusonga.

“Jambo ninaloendelea kuhimiza mimi pesa yangu ninayotafuta kwa wadau wangu mbalimbali  pamoja na mimi mwenyewe nataka nikiitoa nione matokeo chanya maana mimi ni mchumi hivyo lazima tuwe na nia ya dhati  ya kuhakikisha tunapata timu ambayo itacheza ligi kuu mwaka kesho hata kama tukipata timu zaidi ya moja ni sawa tena ni vizuri zaidi alisema na kuongeza.

“Tutaunda uongozi wa mkoa ambao utashirikiana na uongozi wa timu tutawapangia majukumu pamoja na wajibu wao lengo letu ni mafanikio lakini kwa kuwa tuna timu tatu pesa hizo nitazipeleka  zaidi kwenye timu ambayo inaibua vipaji vya ndani tuviendeleze ili wachezaji  wakacheze Taifa Stars,”amesema Malima.

Aliwataka wadau hao kuweka  msingi imara  wa soka  ili wachezaji waweze kucheza mpira mzuri pia  kuendesha club kwa uwazi maana mambo hayo yanasaidia  kuleta mafanikio na matokeo chanya  kwenye soka.

“Hakuna sehemu yenye  majungu kama mpira tunaupenda lakini ni pasua kichwa hivyo uwazi ni jambo la msingi, mafanikio kwenye mpira hayaji kwa kutamani bali ni kujipanga kama nilivyosema awali mpira hauchezwi bila pesa ukicheza bila pesa siku zote utaona mazingaombwe uwanjani maana mchezaji ambaye anamudu mchezo kila siku atakuwa na changamoto  mara atasema mguu unamuuma,”alifafanua  Malima.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza(MZFA), Leonard  Malongo, alisema watashirikiana bega kwa bega na Mkuu huyo wa mkoa ili kuhakikisha mkoa ho unapata timu zitakazoshiriki ligi kuu mwaka kesho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles