26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Upinzani wamteua Fayulu kugombea urais

KINSHASA, DRC

MUUNGANO wa vyama vya upinzani umemtangaza Martin Fayulu, kuwa mgombea wao katika kinyang’anyiro cha urais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, unaotarajiwa kufanyika Desemba 23 mwaka huu ili kumrithi Joseph Kabila ambaye anang’atuka katika kiti hicho.

Vyombo vya habari vimetoa wasifu wa mgombea huyo ambaye anahusishwa moja kwa moja na mataifa mawili makubwa duniani ya Marekani na Ufaransa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Al Jazeera, Fayulu, amewahi kuwa ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya mafuta ya Mobil ya Marekani katika nchi mbalimbali barani Afrika kutoka mwaka 1984 hadi 2003.

Duru za kisiasa za DRC zimemtaja Fayulu kama mtu kutoka nje ya mtandao wa kisiasa nchini humo. Uteuzi wa Fayulu kuwa mgombea wa upinzani nchini DRC umefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Geneva nchini Uswisi.

Kinyang’anyiro cha urais kitawakutanisha Martin Fayulu na Emmanuel Ramazani Shadary, ambaye amewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo.

Aidha, Fayulu, ni miongoni mwa watu mashuhuri waliosimama kidete kupinga hatua ya Rais Kabila kutaka kufanya mabadiliko ili kumwongezea muda wa kukaa madarakani katika muhula mwingine.

Fayulu, anatarajiwa kutimiza miaka 62 ifikapo Novemba 21 mwaka huu, amewahi kukamatwa mara kadhaa kwenye maandamano ya wafuasi wa vyama vya upinzani mjini Kinshasa.

Mwanasiasa huyo anaungwa mkono na wanasiasa wakubwa wawili nchini humo, makamu wa rais wa zamani DRC, Jean-Pierre Bemba, ambaye ameondolewa katika kinyang’anyiro cha urais na gavana Moise Katumbi, aliyezuiwa kuingia DRC kurejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo.

Uteuzi wa Fayulu umehitimisha nafasi ya Felix Tshisekedi, kiongozi wa muda mrefu wa chama cha upinzani cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS). Felix ni mtoto wa mwanzilishi wa chama hicho, Etienne Tshisekedi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,277FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles