29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Upelelezi kesi ya Shamimu, mumewe haujakamilika

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Upelelezi wa kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin inayomkabili mmiliki wa Blogu ya 8020 Fashion, Shamim Mwasha (41) na mumewe mfanyabiashara Abdul Nsembo (45), haujakamilika.

Kesi hiyo imetajwa leo Jumatatu Mei 27, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, ambapo upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon alidai mbele ya  Hakimu Mkazi wa Mfawidhi, Kelvin Mhina kesi lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi haujakamilika, hivyo anaomba tarehe nyingine.

Baada ya kudai hayo Wakili utetezi, Charles Kisoka na Hajra Mungula walidai kuwa shauri hilo halina dhamana hivyo wanauomba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 10, mwaka huu, washtakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu kesi yao haina dhamana.

Washtakiwa hao ambao ni wakazi wa Mbezi Beach, wanatuhumiwa kwa shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles