24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mtafiti ataka wakulima kuliongezea bibo thamani

Florence Sanawa, Mtwara

Mtafiti kutoka taasisi ya kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Naliendele, Regina Msoka amesema kuwa wakulima wa zao la korosho wanapaswa kujua thamani ya bibo ili wayatumie kama sehemu ya kuwaongezea kipato badala ya kuangalia korosho pekee.

Hatua hiyo imekuja baada ya wakulima kutelekeza mabibo shambani jambo lililowafanya watafiti Naliendele kufanya tafiti mbalimbali na kuja na jibu ambalo litawawezesha wakulima kutunza mabibo na kutengeneza aidha juisi au mvinyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mtafiti huyo amesema mkulima anapoacha bibo shambani anapoteza fedha nyingi kuliko hata anapouza korosho.

“Utafiti uliofanywa na taasiisi yetu uliiona kama fursa muhimu kwa uchumi wa nchi yetu itaongeza hamasa ya wawekezaji.

“Unajua bibo ni tunda lenye faida kubwa lakini linatelekezwa shambani ambapo tunatengeneza juisi, jam na mvinyo ambapo kilo moja inauzwa Sh 11,300 kwa hiyo muuzaji hupata Sh 300,000 kwa mabibo kilo tisa unapoyaongezea thamani, kwa hiyo mkulima akipata kilo moja  ya korosho anaacha kilo tisa za mabibo shambani,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles