Upelelezi kesi ya anayedaiwa kuua mkewe kwa kumchoma moto wakaribia kukakimilika

0
381

KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara Hamis Said (38), anayedaiwa kumuua mkewe Naomi Marijani kwa kumchoma na magunia mawili ya mkaa, umedai kwa mara nyingine upelelezi uko hatua za mwisho kukamilika.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon, alidai hayo jana wakati kesi hiyo inatajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally.

Wankyo alidai kesi ilikuja kwa kutajwa, upelelezi uko katika hatua za mwisho kukamilika na kuna maeneo mengine ya kufanyia upelelezi ambayo Mkurugenzi wa Mashtaka nchini kaelekeza yafanyiwe kazi.

Jamhuri waliomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine na mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 7 kwa ajili ya kutajwa. Mshtakiwa yuko rumande.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshtakiwa anadaiwa alitenda kosa la mauaji Mei 15, 2019 katika oneo la Gezaulole Kigamboni, Dar es Salaam ambapo alimuua mtu anayeitwa Naomi Marijani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here