23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

Upande wa mashtaka kesi ya Mwanyika watakiwa kueleza hatua za upelelezi

PATRICIA KIMELEMETA

UPANDE wa mashtaka katika kesi inayomkabili aliyekuwa Makamu wa Rais wa migodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika na wenzake umetakiwa kueleza hatua zilizofikiwa hadi sasa katika upelelezi.

Hayo yalielezwa na Wakili wa utetezi, Rweikama Rweikiza, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mtega, wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Wakili Rweikiza alidai kuwa kumbukumbu zinaonyesha mara ya mwisho upande wa mashtaka ulieleza kuwa upelelezi ulikuwa haujakamilika hivyo Mahakama iliwataka kuja na majibu ya walikofikia katika upelelezi.

Hivyo jana aliiomba tena iwepo kwenye kumbukumbu kama ilivyowekwa mara ya mwisho ambapo upande wa mashtaka walitakiwa waje na majibu kuhusu hatua ya upelelezi ilipofikia.

Awali Wakili wa Serikali, Patrick Mwita, alieleza mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa kwani upelelezi bado haujakamilika hivyo aliiomba tarehe nyingine ili itajwe tena.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Wakili Mwita, aliieleza mahakama hiyo kuwa Jamhuri imesikia madai hayo na itayafanyia kazi.

Baada ya kusikiliza maelezo hayo, Hakimu Mtega, aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 18, mwaka huu.

Mbali na Mwanyika, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Uhusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu, Alex Lugendo, Mkurugenzi Mtendaji wa Pongea, North Mara na Bulyanhuku, Assa Mwaipopo, Kampuni ya Mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 39, yakiwemo ya utakatishaji, kukwepa kodi zaidi ya Dola za Marekani milioni 12, kugushi na kutoa matamko ya uongo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles