23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati za Bunge kuanza Dodoma wiki ijayo

AGATHA CHARLES

VIKAO vya Kamati 14 za Kudumu za Bunge vinatarajiwa kuanza Januari 14 ambavyo vitaendelea hadi Januari 27, mwaka huu jijini Dodoma huku Kamati ya Masuala ya Ukimwi, Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati za Bajeti zikitarajiwa kuanza Januari 7, mwaka huu.

Hayo yalielezwa jana katika taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mawasiliano, Ofisi za Bunge kilichoko jijini humo.

Kilieleza kuwa wakati wa kamati hizo ambazo shughuli zake zimepangwa kwa kuzingatia kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la Januari 2016, moja ya kazi zitakazofanywa ni uchambuzi wa miswada mitano ya sheria iliyopelekwa kwenye Kamati tatu za Kudumu za Bunge pamoja na kupokea maoni ya wadau kuhusu Miswada ya Sheria.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa kazi nyingine ambayo itafanywa ni uchambuzi wa taarifa mbalimbali za Msajili wa Hazina kuhusu uwekezaji wa Mitaji ya Umma katika mashirika na taasisi mbalimbali nchini.

Pamoja na hilo, shughuli nyingine ya tatu itakuwa ni uchambuzi wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu za mwaka wa fedha 2016/2017.

Shughuli nyingine ilielezwa ni uchambuzi wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu hesabu zilizokaguliwa za Serikali za Mitaa za Mwaka wa Fedha 2016/2017.

Aidha, shughuli ya tano itakuwa ni uchambuzi wa taarifa za utekelezaji wa majukumu ya Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali.

Ilielezwa kuwa pia kutakuwa na uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa bungeni wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge.

Shughuli ya saba itakuwa ni maandalizi ya Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati kwa kipindi cha Januari 2018 hadi Januari, 2019.

Pia shughuli nyingine zitahusisha Kamati tatu za Ardhi, Maliasili na Utalii, Kamati ya Kilimo, Kamati ya Mifugo na Maji na Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa ambazo zitakutana pamoja Januari 25, ili kupokea na kujadili taarifa ya kisekta kuhusu Hali ya Migogoro ya Ardhi nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles