24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Unyonyeshaji unavyoweza kuepusha saratani ya matiti, udumavu

Na AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM

KILA mwaka ifikapo Agosti 1 hadi 7 dunia huadhimisha wiki ya unyonyeshaji ili kuha- masisha njia salama itakayoweza kumkinga mtoto na maradhi. Kulingana na Utafiti wa Hali ya Lishe

nchini wa mwaka 2018, takribani asilimia 97 ya watoto wenye umri chini ya miaka miwili wananyonyeshwa maziwa ya mama.

Idadi ya watoto wanaoanzishiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa wakati sahihi katika kipindi kisichozidi saa moja baada ya kuzaliwa ni asilimia 53 ikilinganishwa na asilimia 51 ya mwaka 2015/2016.

Idadi ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kupewa maji, vinywaji na vyakula vingine katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa ni asilimia 58.

Idadi ya watoto wanaoanzishiwa vyakula vya nyongeza kwa wakati sahihi katika umri wa miezi 6 hadi 8 ni asilimia 87.

Idadi ya watoto wenye umri wa miezi 6 – 23 wanaolishwa chakula kinachokidhi vigezo vya ubora kilishe ni asilimia 35 huku kiwango hiki kikiongezeka ikilinganishwa na asilimia 10 kwa mwaka 2015/2016.

Vigezo hivyo ni idadi sahihi ya milo anayopewa mtoto kwa siku kulingana na umri wake na mlo kuwa na mchanganyiko wa vyakula kutoka kwenye makundi yasiyopungua manne ya vyakula.

Umri wa miezi 6-23 hupewa vyakula vya nyongeza kwa kuzingatia vigezo muhimu vya umri, kiasi, idadi ya milo kwa siku, uzito na ulaini wa chakula na mchanganyiko wa vyakula mbalimbali.

Vigezo vingine ni pamoja na kuzingatia kiasi cha chakula anachopewa mtoto kulingana na umri wake, uzito na ulaini wa chakula na mchanganyiko

wa nyakula mbalimbali, bila kusahau usafi na usalama wa chakula wakati wa kutayarisha mlo wa mtoto.

UMUHIMU WA KUNYONYESHA

Ofisa Lishe Mtafiti Kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Fatma Mwasora, anasema kuna umuhimu mkubwa wa mama kumnyonyesha mtoto maziwa pekee bila kumchanganyia na maziwa ya ng’ombe.

“Maziwa ya mama ni muhimu kwa mtoto kwa sababu ni chakula na kinywaji pekee kinachotosheleza mahitaji ya lishe ya mtoto tangu anapozaliwa hadi anapotimiza umri wa miezi sita,” anasema.

Anasema maziwa ya mama hukinga mwili wa mtoto dhidi ya maradhi/magonjwa na kwamba ndiyo yenye uwezo wa kumpatia mtoto kinga.

“Husaidia kuimarisha taya pamoja na misuli ya ulimi na masikio ya mtoto hali hii husaidia kupunguza maradhi ya masikio kwa mtoto, kuboresha uwezo wa kuanza kutamka maneno kwa mtoto na kumlinda dhidi ya maradhi ya meno na kupunguza uwezekano wa kupata matatizo mengine ya kinywa.

Mwasora anasema maziwa ya mama yana virutubishi vinavyojitosheleza ambavyo humsaidia mtoto kwa ukuaji na maendeleo katika uwiano ulio sahihi.

“Maziwa ya mama pekee ndiyo yanaweza kumpatia mtoto sehemu kubwa ya vitamin A anayohitaji hata wakati wa mwaka wa pili wa maisha yake,”anasema.

Anasema mtoto akinyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila hata maji humsaidia kupata madini chuma ya kutosha na humkinga na upungufu wa wekundu wa damu hadi anapotimiza umri wa miezi sita.

Mwasora anaeleza kuwa maziwa ya mama huyeyushwa kwa urahisi na kutumika kwa ufanisi.

“Mafuta yaliyopo kwenye maziwa ya mama huyeyushwa na kufyonzwa kwa ufanisi zaidi kwenye mwili wa mtoto kuliko yale yaliyopo kwenye maziwa ya ng’ombe au maziwa ya kopo kwa ukuaji wa ubongo, macho na mishipa ya damu ya mtoto,”anasema.

Mwasora anasema ipo tofauti kubwa kati ya maziwa ya mama na ya ng’ombe hasa katika suala la ulishaji watoto wachanga na wadogo.

“Elimu inabidi itolewe kwa wajawazito na akina mama wanaonyonyesha kutambua umuhimu wa kutochanganya maziwa ya mama na maziwa ya ng’ombe pindi mtoto anapolishwa,” anasema.

Anasema maziwa ya wanyama kama ng’ombe na ya mama yana tofauti kubwa katika kiasi cha protini, sukari na nishati.

“Jamii ielewe kuwa wanyama (mfano ng’ombe) hukua haraka hivyo, wanahitaji protini nyingi zaidi katika ukuaji wao. Pia jamii ielewe kuwa kiasi cha protini katika maziwa ya wanyama ni kikubwa sana.

“Endapo mtoto wa binadamu atapewa maziwa hayo ni vigumu kwa figo kutoa mabaki ya protini ya ziada kwenye mwili yanayotokana na maziwa ya wanyama,”anasema.

Anasema matumizi ya maziwa ya wanyama mfano ya ng’ombe kwa mtoto mchanga yanamuweka mtoto katika hatari ya kupata matatizo ya figo na viungo vingine.

“Protini nyingi iliyopo kwenye maziwa ya ng’ombe pia hufanya mgando mzito usioyeyuka kwenye tumbo la mtoto hivyo mtoto anaweza kukosa choo na kupata maumivu ya tumbo,”anasema.

Anasema wakati mwingine watoto wachanga hushindwa kustahimili protini ya maziwa ya wanyama hivyo kupata mzio (aleji) baada ya kuyatumia.

“Kiasi kikubwa cha protini ya ‘whey’ (kwa lugha ya kitaalam) kwenye maziwa ya mama ni muhimu kwa mtoto mchanga kwani yana viini ambavyo humkinga dhidi ya maradhi mbalimbali,” anasema.

Anasisitiza kuwa maziwa ya wanyama na yale ya kopo hayana viini vya kumkinga mtoto dhidi ya maradhi.

Mwasora anasema maziwa ya mama yana kimeng’enyo kinachomsaidia kuyeyusha mafuta hivyo, kufyonzwa kwa ufanisi na mwili wa mtoto kuliko yale yaliyopo kwenye maziwa ya ng’ombe au maziwa ya kopo maalumu kwa watoto wachanga.

Pamoja na kuendelea kunyonyeshwa maziwa ya mama au maziwa mengine Mwasora anasisitiza kuwa mlo wa mtoto usikose chakula cha asili ya wanyama.

Ingawa tumeweza kupiga hatua katika kuboresha viwango vya unyonye- shaji, bado jitihada zaidi zinahitajika ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali nchini ili kuhakikisha tunafikia viwango bora vya ulishaji watoto ikiwemo unyonyeshaji.

MAELEKEZO YA WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO), linaelekeza watoto kunyonya maziwa ya mama pekee katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa.

Kwa mujibu wa WHO asilimia 58 ya watoto walio chini ya miezi sita ndio hunyonyeshwa maziwa ya mama pekee pia inaelekeza kuwa mtoto anapotimiza miezi sita ni vyema kuanzishiwa aina nyingine ya vyakula ili kumwepusha na hatari ya kupata utapiamlo.

Aidha Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa mwaka 2018 linaonyesha kuwa watoto 4 tu kati ya 10 ndio hunyonyeshwa maziwa ya mama katika miezi sita ya mwanzo ya maisha yao sawa na asilimia 41 ya watoto wote.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo nchi zinazoendelea ndio zinaongoza kwa un- yonyeshaji huo Rwanda ikishika nafasi ya kwanza kwa asilimia 86.9, ikifuatiwa na Burundi (82.3), Sri Lanka (82), Visiwa vya Solomon (76.2) na Vanuatu (72.6).

Ripoti hiyo inaonyesha watoto katika maeneo ya vijijini wana kiwango ki- kubwa cha kunyonyeshwa kuliko mijini.

UNICEF inakadiria kuwa kuongeza kiwango cha unyonyeshaji kutazuia vifo 823,000 kila mwaka vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano na vifo 20,000 kila mwaka vitokanavyo na saratani ya matiti kwa kina mama.

Idadi ndogo ya watoto wananyonyeshwa wanapozaliwa ambapo takwimu mpya za UNICEF kwa mwaka 2018 zinaonyesha chini ya nusu ya watoto wote duniani au asilimia 43 ndio walioweza kunyonyeshwa katika saa ya kwanza ya uhai wao baada ya kuzaliwa.

USAFI WAKATI WA UNYONYESHAJI

Daktari Raymond Mgeni kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya anasema ni muhimu mama kuzingatia usafi wakati wa unyonyeshaji.

“Mtoto anapozaliwa kinga ya mwili wake ndio inazidi kukua kwahiyo mama asipozingatia usafi wakati akinyonyesha anaweza kumsababishia mtoto maambukizi ya bakteria ambao husababisha athari,”anasema.

Wakati wa unyonyeshaji Dk. Mgeni anasema mama anapaswa kuwa nadhifu kwani wapo bakteria ambao huishi katika ngozi hivyo usafi usipozingatiwa unaweza kuleta shida kwa mtoto.

“Kila mama anaponyonyesha usafi ni muhimu pia wakati wa kunyonyesha anapaswa kumuangalia mtoto kama amelala kwa sababu akiendelea kumnyonyesha huku akiwa amelala mtoto anaweza kupaliwa”anasema.

LISHE KWA WATOTO

Mwakilishi wa Shirika la Save the Children, Judith Kimambo, anasema katika kuhakikisha wanakabiliana na udumavu kwa watoto katika siku 1,000 za maisha ya awali ya mtoto wameanzi- sha miradi kusaidia lishe kwa watoto.

“Tuna miradi Dodoma, Rukwa, Zanzibar, Iringa, Morogoro na tume- kuwa tukitoa elimu kwa maofisa kilimo, wahudumu wa afya, watendaji wa vijiji mpaka ngazi ya chini namna ya kukabiliana na udumavu kwa watoto hasa kwa kuhamasisha masuala ya lishe na unyonyeshaji,” anasema.

Anasema shirika hilo limekuwa likitoa elimu kwa wananchi ngazi ya jamii namna bora ya unyonyeshaji, ulaji unaofaa na familia kushirikiana katika suala la lishe.

Ripoti ya Shirika hilo inaonyesha utapiamlo unaochangiwa na kutonyonyeshwa ipasavyo unakadiriwa kusabisha vifo vya watoto 2.7 kila mwaka.

IMANI POTOFU

Hasna Fadhili ni mkazi wa Mbagala, anasema miongoni mwa nadharia am- bazo watu wamekuwa wakizizungumza ni kuwa maziwa ya kwanza ya mama si mazuri kwa mtoto yanapaswa kum- wagwa kwani kunyonyesha humfanya mama anenepe kupindukia.

Anasema wengine huamini kuwa maziwa ya mama pekee hayawezi kumridhisha mtoto wa umri wa miezi 0 hadi sita huku wengine wakiamini kuwa baadhi ya vyakula si vizuri kwa wanawake wanaonyonyesha.

“Wengine wanasema ukimyonyesha maziwa ya mama pekee ni hatari kwani mtoto atapata kiu hivyo, lazima anywe maji mara baada ya kuzaliwa, mbali na hilo wengine hudhani ukimnyonyesha mtoto matiti yatalala,” anaeleza Hasna

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles