25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Unicef yataka haki za wanawake, watoto

 CHRISTINA GAULUHANGA– DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (Unicef), limeviomba vyombo vya habari pamoja na wadau wake kuzingatia haki za wanawake na watoto katika matangazo kwenye vyombo hivyo ili kuondoa unyanyapaa katika jamii inayowazunguka.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Mshauri Mkuu wa Masuala ya Sayansi ya Jamii na Mshauri wa Kimataifa, Dk. Johanna Maula, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu haki za wanawake na watoto kwenye matangazo mbalimbali yanayotolewa.

Alisema ni wakati sasa wa kutafakari kama matangazo hayo yanazingatia haki hizo ili kulinda jamii na kizazi kijacho.

 “Ni vema tukajiuliza katika kuripoti Matangazo haya kuna unyanyapaa kwa wanawake na watoto na hali ikoje kwenye vyumba vya habari endapo linaletwa matangazo kama hayo je kuna dawati maalumu la kuzingatia haki inatekelezeka,”alisema Johanna.

Alisema lengo kuu ni kutengeneza mfumo maalum wa jinsi ya kuripoti na kutangaza habari za wanawake na watoto.

Naye, Ofisa kutoka Unicef, Dorosella Bishanga alisema ni muhimu kuzingatia genda wakati wa uandishi na utangazaji wa habari na matangazo mbalimbali.

Wakichangia mada hiyo baadhi ya waandishi kwa nyakati tofauti walisema, matangazo mengi yanaonyesha wanawake ni watu wa kupokea jambo ambalo si kweli.

Walishauri Unicef kuangalia namna bora ya kutengeneza mkakati wa kutangazamatangazo hayo ikiwashirikiana na wanahabari, watunga sera, serikali pia na mawakala.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles