25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

CCM wahimiza uchaguzi wa haki

MWANDISHI WETU– CHATO

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Bara, Galila Wabanh’u amesema kuwa chama hicho kinataka kuona Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu unakuwa huru na haki.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa CCM huwa na utaratibu wake wa namna ya kuwapata wagombea wake kwa ngazi hizo za udiwani, ubunge na urais hivyo wanaamini haki itatendeka kwa kila upande. 

Galila ambaye ni MNEC anayetokana na Jumuiya ya Wazazi wa CCM, alitoa kauli hiyo jana wilayani Chato mkoani Geita, katika mkutano wa ndani uliowashirikisha wajumbe wa mabaraza ya wilaya jumuiya zote za chama, viongozi wa chama na serikali, ambapo waliwakumbusha viongozi hao kutenda haki kwa wanachama oet watakaojitokeza kuwania nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho.

“Tuepuke mizengwe baina yetu na tusikubali kupiga kura kwa misingi ya rushwa kwani kwa kufanya hivyo mtajikosesha uhalali wa kuhoji maendeleo. Diwani au mbunge akichaguliwa kwa rushwa tafsiri yake mlimuuzia kura hivyo ana haki ya kutowajibika kwa kuwaletea maendeleo na kuwatatulia kero. Tuwe waangalifu kwenye kuchagua viongozi wetu,” alisema Galila. 

Kutokana na hali hiyo aliwataka kuwa waungwana kwa kuwaunga mkono wawakilishi wao waliofanya vizuri katika miaka mitano inayomalizika sasa 2015-2020 na kuwakataa waliofanya vibaya. 

“Uungwana ni vitendo, wapo madiwani na wabunge waliotimiza wajibu wao tuwaunge mkono katika uchaguzi huu. Kwa wale waliowasahau na kuwatelekeza vuteni subira chama kitoe utaratibu wa uchaguzi, hao msiwachague maana watakuwa mzigo kuwauza kwa wananchi,” alisema 

Akiwa katika ziara yake hiyo ya siku 14 katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, Mjumbe huyo wa NEC, alikabidhi ndoo mbili za rangi na kuungwa mkono na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Batholomeo Manunga aliyekabidhi ndoo mbili hivyo kukamilisha ndoo nne za rangi zilizohitajika kwa ajili ya kupaka rangi nje jengo la ofisi za CCM wilaya.

Pia aliwahamasisha CCM na jumuiya zake kuhakikisha wanakamilisha miradi waliyoibuni ili waweze kufanya siasa kwa kujiamini na ufanisi zaidi.

Katika kuunga mkono ujenzi wa mradi wa jumuiya ya wazazi wilaya hiyo ya kujenga nyumba ya wageni Galila alichangia tofali 500 ambapo aliungwa mkono na viongozi mbalimbali akiwamo Mkuu wa hiyo, Charles Kabeho ambaye alichangia matofali 100, CCM wilaya hiyo matofali 200.

Hata hivyo aliwataka wanachama na viongozi kuendelea kuyasemea mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2015-2020 katika maeneo yao pamoja na kudumisha umoja na mshikamano uliopo ndani ya chama na serikali. 

Katika ziara yake hiyo Galila, ameambatana na Katibu wa Oganizesheni wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Chollaje Mohamed

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles