24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yasema nchi ina mafuta yakutosha

 MWANDISHI WETU– DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, amesema kuwa nchi ina ziara ya mafuta ya kutosha bila kuwa na tatizo.

Hayo aliyasema mwishoni mwa wiki jijini Dar e Salaam, alipokuwa akikabidhi tuzo zilizoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania kwa watoa huduma wake mwaka 2019.

Alisema kuna ziada ya mafuta ya dizeli ya siku 28 lita milioni 197, petroli ziada ya lita 97.04 kwa siku 38 na mafuta ya ndege ziada ya lita milioni 30.9 kwa siku 56, hivyo hakuna hofu katika nishati hiyo.

Kutokana na hali hiyo alimpongeza Rais John Magufuli kwa usimamizi mzuri wa sekta ya nishati na kusimamia uanzishaji wa mfumo wa kuagiza mafuta kwa pamoja.

Pia aameitaka Kampuni ya Puma Energy Tanzania Limited kupeleka huduma zake katika mikoa yote nchini na hasa maeneo ya vijijini.

Alisema kwamba sera ya serikali ni kupeleka nishati za umeme, gesi na mafuta katika maeneo mbalimbali yakiwamo ya vijijini.

“Maagizo yangu ni kwamba mfike mikoa yote nchini ambayo hamjafika ili ipate huduma. Najua hamjafika Katavi, Rukwa, Kigoma, Geita, Mara, Simiyu. Nendeni mikoa hiyo,” alisema.

“Sera yetu ni kufikisha nishati vijijini. Nishati hizo ni umeme, gesi na mafuta. Kwa gesi tumefanya vizuri sana na umeme unaendelea kusambazwa vijijini. Ninyi vituo vya mafuta vijijini bado tuko nyuma. Anzisheni vijijini sio mijini,” alisema Dk. Kalemani

Alisema si jambo jema kuona wananchi wanabeba mafuta katika madumu au chupa za maji za plastiki huku yakihifadhiwa nyumbani jambo linalohatarisha usalama wa wananchi.

Aidha, aliwaagiza kuongeza ushindani, huku akiwapongeza kwa kutoa ajira 149 za kudumu kwa Watanzania na za jumla takribani 800 kwa wazawa.

Dk. Kalemani alitoa shukrani kwa bodi na menejimenti kwa kusimamia ajira hizo na kuhakikisha Watanzania wengi wanaajiriwa katika kampuni hiyo.

Puma Energy Tanzania Limited inamilikiwa kwa asilimia 50 na Serikali ya Tanzania kupitia Msajili wa Hazina na Kampuni ya Puma Investments Limited.

Kutokana na hilo, aliipongeza kwa kutoa gawio kwa Serikali ambalo limekuwa likiongezeka kutoka shilingi bilioni 9.0 mwaka 2018 na shilingi bilioni 11.0 mwaka jana. Aliwataka mwaka huu waongeze kufikia zaidi ya shilingi bilioni 13.

Aidha aliwapongeza wadau wote wanaoagiza mafuta kwa pamoja kwa kuiwezesha nchi kuwa na mafuta ya kutosha kila wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles